Mabalozi wa nchi za afrika wakutana na naibu waziri wa mambo ya nje china kuzungumzia ubaguzi wanaofanyiwa waafrika china

Mabalozi
wa Nchi za Afrika wamekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje China,
Chen Xiaoding kuzungumzia changamoto zinazowakabili baadhi ya raia wa
Afrika katika mji wa Guangzhou.


Chen amewaeleaza Mabalozi kwamba Serikali ya China haiungi mkono vitendo vya ubaguzi dhidi ya yeyote.


Kuhusu changamoto zilizowasilishwa na Mabalozi wa Nchi za Afrika
zinazowakabili Waafrika nchini China, China imesema Mamlaka ya Jimbo la
Guangdong itachukua hatua kuzishughulikia ikiwemo Raia wa Afrika ambao
wameondolewa kwenye makazi na hoteli kupatiwa makazi mbadala ya muda.
China imewaahidi Mabalozi wa Nchi za Afrika kuwa itahakikisha zoezi la
udhibiti wa corona linaendeshwa kwa usawa, kutoa elimu kwa umma ili
kuepuka hatua zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni ubaguzi na Kuanzisha
mtandao wa mawasiliano kati ya Mamlaka za Nchi hiyo na Ofisi za
Kibalozi.