Mabasi yanayotumia umeme yafanyiwa majaribio

Haya ni mabasi yanayoenda kwa kutumia nishati ya umeme. 


Mabasi haya aina ya Yuton yametengenezwa nchini China na yameanza kufanyiwa majaribio katika mji wa Athens, Ugiriki huku usimamizi wa mji huo ukizingatia kuiga matumizi ya mabasi yanayotumia umeme kuboresha usafiri kwenye mji huo.