Madereva lusahunga wataka kumuona rais magufuli

Na Clavery Christian Biharamulo.

Kufuatia ajali za mara kwa mara katika barabara ya Lusahunga kwenda mpakani mwa Tanzania na Burundi baadhi ya madereva  wa magari makubwa ya  mizigo wameiomba  Serikali
kuwatengenezea barabara hiyo ili kuwaondelea adha wanayokutana nayo.
kwa mujbi wa Madereva hao, kutokana na ubovu wa barabara hiyo wamekuwa wakilazimika kusafiri kwa kutumia saa nane mpaka kumi katika eneo la
Lusahunga kwenda Benako kufuatia barabara hiyo kujaa mashimo makubwa
yanayopelekea magari yao kuharibika vibaya na kuanguka na kuwasabishia
ulemavu na wengine kupoteza maisha wanaopona hufukuzwa kazi na mabosi wao.


Barabara  ya Lusahunga  hadi  Lusumo  wilayani  Ngara
mkoani Kagera inatumika kusafirisha bidhaa mbalimbali  kwa
kutumia  malori makubwa  ya mzigo kwenda nje ya nchi licha ya barabara
hiyo kuongeza pato la taifa imekuwa haipitiki kutokana na kuwa na
makorongo na mashimo yanayopelekea magari kuanguka kwa kupata
ajali zisizokuwa za lazima.
wakiongea na APC blog wamesema kuwa kufuatia ubovu wa barabara hiyo umepelekea  msongamano
wa malori kupaki ovyo ovyo njiani kutokana na kupata kuharibika kwa
magari hayo mengine yakianguka na kukata baadhi ya vyuma huku wakihofia
usalama wa maisha yao na magari waliyo nayo kwani mda mwingine gari
linaharibikia sehemu ambapo hakuna hata mtu yeyote wa kukupa msaada.
APC blog imefanikiwa kuzungumza na baadhi ya madereva  ambapo wametoa kilio
chao na wengine wakiomba kukutana na Rais Dkt John Magufuli ili kumueleza kero ya
barabara  hiyo  ambayo imekuwa sintofahamu kwao.
Mbali
na madereva kulia na ubovu wa barabara hiyo  abiria wanaosafiri kutoka
mikoa mbalimbali  kupita barabara hiyo  wamesema kuwa baadhi ya wamama
wajawazito wamekuwa wakijifungulia kwenye gari  kabla ya muda wao kutokana na
kurushwa rushwa kwenye mashimo.