Mongela ameyasema hayo leo wakati akizungumza na madiwani wa Jiji la Arusha pamoja na wakuu wa idara wa Jiji hilo katika kikao cha kujadili hoja za mkaguzi mkuu wa serikali CAG.
Rc Mongela amesema kwamba Jiji hilo lina kila aina ya vyanzo vya mapato ambavyo madiwani hao wangevitumia vyema wangeweza kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 50 kila mwaka wa fedha lakini imekuwa tofauti na badala yake wamekuwa ni watu wa kutengenezeana majanga.
“Jiji la Arusha Mnakusanya shilingi Bilioni 20.3 na hazitoshi hata kuwaendeleza nyie wenyewe lakini mnapata ruzuku ya shilingi Bilioni 66, Sasa hayo hamyaoni mmebaki kukalia majungu, kunafikiana na kushikiwa akili na baadhi yenu mnasahau kazi za wananchi wenu”. Alisema mongela.
“Nilisema Jiji likusanye shilingi Bilioni 43 lakini nilivyo safiri nikarudi nilikuta wamechakachua hadi Bilioni 33 ili waweze kutupiga hizo zingine, uwezo wa kukusanya hadi shilingi Bilioni 50 kwa mwaka uwezo upo cha ajabu mnashikiwa akili”. Aliongeza Mongela.
“Mjitafakari sana, maana milioni 200 mnataka kuuwana maana nasikia kila mahali mnapiga tu sio mizani wala wapi, Mkibadikika mtakusanya mapato mengi zaidi na itakuwa ni rahisi kwenu nyie kupanga fedha hizo zikaendeleze maeneo yapi ya kata zetu na wananchi waweze kunifuika”. Alisisitiza Mongela.
Aidha Rc Mongela alieleza wamezuia vibali vya kusafiri kwa madiwa hao kwa kipindi hiki cha sasa hadi miaka yao itakapo kwisha ili waweze kufanya kazi za wananchi na halmashauri hiyo kuwa sawa kuondokana na harufu zote za ufisadi.
“Kwasasa hatuwezi kupitisha kibali chochote cha kusafiri hadi miaka mitano hii iishe, mtazunguka humu ndani hadi mtachakaa”. Alisema Mongela.
“Kunawakati naamua kuwaacha makusudi maana naamini nyie wote ni watu wazima kama mtakaa kwa kuburuzwa na mtu anatoka huko nyumbani kwake anakuja kuwashikia akili”. Alisisitaza Mongela.
“Juzi alinifata Mbunge, kuomba lile eneo la kaloleni tuwajengee wamachinga nadhani Mbunge bado hajanielewa wala na mimi sijamuelewa kabisa maana hatuwezi kuweka machinga kila eneo kwasasa, tujenge masoko ya maana na yenye hadhi na ndipo baadae tuwahamishe taratibu”. Alisisitiza Mongela.
Mongela alieleza kuwa katika suala la maendeleo na ikishafika hatua kuna maslahi ya taifa hakuna tena kubembelezana maana kinacho takiwa ni maendeleo na kuwaonya watakao jifanya vinara na wakikukutwa hakuna atakaye wasaidia wote watamkimbia.
Mbali na kuwa mkali Mongela juu ya kukwerwa na madudu yanayo endelea katika halmashauri hiyo ya Jiji la Arusha alimtahazalisha kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo Agney Chitukulo kuwa makini na madiwani hao maana hawatabiliki na wanaweza kumtengenezea fitna wakati wowote.
“Nikuombe Mkurugenzi utusaidie katika safu ya utendaji, maana katika eneo jingine bovu ni kwa watendaji ili kuweza kufanya majukumu yao kwa weledi na kwa manufaa ya nchi na uwe makini sana na hawa madiwani hawachelewi kukuwekea maneno na kukutafutia balaa”. Alisema Mongela.
Aidha Mongela aliwataka madiwani hao kubadilika na kuacha majungu ili kuweza kukidhi hadhi ya watanzania na kukidhi hadhi ya Jiji na kuwa na maendeleo na kumtaka Meya wa Jiji hilo Maximilian Iraqe kuwa weka pamoja madiwani hao ili ifikie hatua ya kuwa pamoja kama madiwani.
“Miezi mitatu iliyopita mlianzisha ajenda ya kutoa Meya kisa mambo yenu ya ajabu ya kuchongeana na ndiyo maana nilisikiliza nikawa nasubilia nione mwisho wake maana kama ni uchaguzi ningepanga mimi ila pia ningefikilia namna nyingine ili kukata mzizi wa fitna na umbea wenu”. Alieleza Mongela.
“Mstahiki meya na madiwani niwaombe tu muwe kitu kimoja mkubaliane na kwenye vikao vyenu muwe na maamuzi ya pamoja mkiendelea na haya mambo yenu kwa mamlaka niliyonayo na kulinda amani nitafungia vikao vyenu maana havina faida kwa wananchi na kama mkiendelea kutafutiana matatizo”. Alisema John Mongela.
Pia Rc Mongela hakuishia hapo aliwaonya vikali madiwani hao juu ya mgogoro wa eneo la Bondeni City ambalo wamekuwa vigeu geu kila kukicha na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja maana kwa kuzidi kuwa vigeu geo mradi huo wa ujenzi wa eneo la Bondeni City inaweza kufa.
“Juzi mmekuja na jambo la Bondeni City isimame ili muanze kuchunguza upotevu wa hekali kadhaa na alivyo kuja waziri wa Ardhi nikatoa tamko langu mbele ya waziri na mbunge wenu kwamba mimi nimekuta swala la Bondeni City”. Alisema Mongela.
Pia Mongela alieleza kwamba zimesha fika timu zaidi ya nne na jiji wakasaini mkataba wa kwanza na badae wakaja kusaini mkataba wa pili na kutaka kulipwa 10% ya fedha na baada ya muda tena wakataka wagawane ardhi na akawambia wamesaini MOU na hadi Benki ya Dunia imeweka eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya mabasi.
“Rais Mhe, Samia Suluhu Hassan, ameirudisha Arusha ile ya zamani hapa sasa tuna tarajia kupata watu maarufu kuja kufanya mkutano mkubwa wa CAF na tumepanga tuwaombe watujengee viwanja vya mpira kule bondeni city nyie bado hamjafikilia chochote juu ya hilo matokeo yake ni migogoro tu”. Alisema Mongela.
“Niwatake msilishwe matango pori badala yake kila mmoja aje na hoja ya maendeleo ya kata yake ila mkiendelea kulishwa maneno na kujifanya mnajua mtajikuta miaka hii mitano imekata na hauna cha kusema kwa wananchi”. Aliongeza Mongela.
“Kwa namna madiwani mnavyo lipeleka hili swala la bondini city huo mradi unaweza kufa maana wafadhili hawawezi kupeleka fedha sehemu zenye migogoro na ndiyo maana nawaeleza ukweli msipo jitafakari kwa kina ujenzi wa hiyo stendi mta uuwa wenyewe na wananchi watakosa stendi kwa maendeleo yao”. alisisitiza John Mongela.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo alitoa wito wa jumla kwa madiwani wote kuacha magenge uchwara ambayo hayata wavusha na maisha ya uonho hayana mwenyewe wakumbuke ubinadamu na maslahi ya taifa kwa ujumla wake.
“Niwaombe madiwani wote kuweni kitu kimoja na muongee lugha moja na hiyo itawasaidia sana niwaombe tu acheni mambo yasiyo na tija kwa jamii wala kusaidia jamii kaeni chini muwe na maamuzi kama viongozi na msitengenezeane matatizo”. Alisema Mongela.
“Imefika hata sasa naangaika na mambo ya wilaya zingine wanao jielewa na kufanya maendeleo kwa wananchi siku nyie mkiacha majungu na maneno maneno mtakuja kuwakuta wenzenu wamepiga hatua zaidi ya maendeleo”. Alimaliza mongela.