Marekani yakiri wanajeshi wake 11 walijeruhiwa na makombora ya iran

Licha
ya Marekani  hapo awali kudai kuwa hakuna askari wake  aliyeuawa au
kujeruhiwa katika mashambulizi 22 ya Makombora ya  Iran dhidi ya kambi
mbili za kijeshi za nchi hiyo huko Iraq, lakini hivi sasa imefichuka
kuwa, wanajeshi kadhaa wa Marekani  walijeruhiwa vibaya na wakupelekwa
kwa usafiri wa ndege katika nchi za Ujerumani na Kuwait kwa ajili ya
matibabu.

Hapo
jana, maafisa wa Marekani walilazimika kukiri juu ya kujeruhiwa
wanajeshi wa nchi hiyo na makombora ya Iran, licha ya hapo awali
kukataa  kuwa kulikuwepo na majeruhi katika shambulizi hilo

Masaa
machache baada ya Iran kuvurumisha makombora na kupiga kambi mbili za
Marekani nchini Iraq, Rais Donald Trump alijitokeza na kudai kuwa, “Ni
furaha kuwatangazia Wamarekani kuwa hakuna askari wetu hata mmoja
aliyeuawa au kujeruhiwa katika shambulizi la makombora la Iran nchini
Iraq.”
Several US service members were
injured during last week’s Iranian missile attack on Al-Asad airbase in
Iraq despite the Pentagon initially saying that no casualties had taken
place https://t.co/zSgAxc0d2h pic.twitter.com/E1AyXPAqna

— CNN Breaking News (@cnnbrk) January 17, 2020