Mbunge charles kimei atoa mashuka 50 kituo cha afya himo

Mbunge wa jimbo la Vunjo Dkt Charles Kimei amekabidhi msaada wa shuka za kujifunika wagonjwa zipatazo 50 katika kituo cha afya Himo huku akiahidi kushughulikia gari la kubeba wagonjwa ili kuondoa kero inayowakabili wagonjwa wanaoenda kupatiwa matibabu.

“Suala la gari la kubebea wagonjwa nimelipokea na niwaahidi kuwa ninalifanyia kazi kituo hiki kinahudumia wagonjwa kutoka kata tatu hivyo ni lazima kiongezewe uwezo”Dkt Charles Kimei mbunge wa Vunjo
“Tunaishukuru serikali kwa jitihada mbali mbali ambazo zinaendelea kufanyika hususani katika kuboresha sekta ya afya ila Vunjo tunavyo vituo vitatu tu vya afya Kati ya kata 16 hivyo tunao uhaba”Dkt Charles Kimei mbunge wa Vunjo