Mbunge mtaturu aanza kutekeleza ahadi zake

 

Mbunge
wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu Novemba 26 ametembelea kijiji cha
Munkinya kukagua kazi ya uchimbaji wa kisima kirefu kinachotarajiwa
kuondoa changamoto ya Maji katika Kijiji Cha Damankia,Samaka na
Munkinya.


Akizungumza
Mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Mtaturu amemshukuru Rais
Dkt John Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuondoa tatizo la maji kwa
wananchi.


Amesema kazi hiyo ilianza Mwaka jana baada ya serikali kuidhinisha kiasi cha Sh Bilioni 3.7.


“Huu
ni muendelezo wa kazi iliyoanza mwaka jana baada ya serikali kutupa
mgao wa fedha kwa ajili ya kuchimba visima 15 kwenye jimbo letu la
Singida mashariki,na mpaka sasa tayari vijiji 13 vimeshachimbwa visima
na miundombinu inaendelea kujengwa ili wananchi waanze kutumia maji safi
na salama,”alisema.


Amewahakikishia
wananchi kupitia Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
2020-2025 kuwa serikali imejipanga kumalizia vijiji vilivyobakia kwa
kuvifikishia maji safi na ikiwa ni kampeni maalum ya kumtua mama ndoo ya
maji kichwani.


Amewaomba
wananchi kutunza miradi hiyo inayojengwa kwa ajili yao ili iweze kudumu
kwa muda mrefu na iwe na faida kwao na kwa vizazi vijavyo.