Mchungaji amuua mkewe kanisani kisa mchepuko kanisani


MCHUNGAJI mmoja nchini Kenya amemuua mkewe, Ann Mghoi,  kwa kumchoma visu, kisha na yeye kujiua.


Mchungaji huyo aliyefahamika kwa jina la
Elisha Misiko alimuua mkewe ndani ya kanisa lake lililopo katika kijiji
cha Chembani, Kisauni, Mombasa na baadaye kujikata koo hadi kufa.

Misiko aliyekuwa mchungaji wa kanisa la
Goods for God’s Gospel Ministries ameacha ujumbe unaomlaumu mkewe kwa
kuwa na mahusiano na kijana mdogo katika kanisa hilo, lakini pia katika
ujumbe huo amemlaumu mkewe kwa kumzuia kuwaona watoto wao.

Mmoja wa polisi wa Kisauni, Julius
Kiragu, ameeleza kuwa mchungaji huyo ameacha makaratasi 17 yaliyoandikwa
kama wosia wake akibainisha sababu za kuchukua maamuzi hayo. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *