Rpc ataja chanzo mlipuko wa moto kigamboni

Kamanda
wa Polisi Temeke, Amon Kakwale, amesema chanzo cha moto uliotokea usiku
wa kuamkia leo katika matanki ya mafuta ya kampuni ya Lake Oil, eneo la
Kigamboni, umesababishwa na hitilafu ya mota inayosukuma mafuta kutoka
chini na kupandisha juu, iliyopelekea cheche na kuleta mlipuko.

Kamanda
Kakwale amesema licha ya kufanikiwa kuuzima moto huo, Askari mmoja wa
Jeshi la Zimamoto alipata mshituko baada ya kuingia kwenye chemba moto
ulikoanzia na kuuzima.

“Mota
ilipata hitilafu za kiufundi ambayo ilizalisha cheche za moto kutoka
kwenye chemba ndogo ya chini, madhara yaliyotokea ni mwenzetu wa uokoaji
mmoja, moshi ulimuingia kwenye kinywa na kupata mshituko kidogo”
amesema Kamanda Kakwale.

Aidha
Kamanda Kakwale ameongeza kuwa hadi sasa bado uongozi wa kampuni ya
mafuta ya Lake Oil, haijawapelekea ripoti kamili inayoonesha ni athari
kiasi gani imetokea