Mkuu wa wilaya ya hai, lengai ole sabaya aamuru viongozi wanne wa chadema wakamatwe

Mkuu
wa wilaya ya Hai, Mhe. Lengai Ole Sabaya ameagiza viongozi wanne wa
CHADEMA mkoani Kilimanjaro akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Lucy
Owenya kukamatwa baada ya kutembelea shule ya Sekondari Rundugai
wilayani humo kwa madai ya kufanya siasa kinyume cha utaratibu.

Wengine
waliokamatwa ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu, Katibu
wa Mbunge wa Hai, Irene Lema na Diwani wa Machame kaskazini, Clement
Kwayu.

Sabaya amesema kuwa viongozi hao walikwenda katika shule hiyo leo Ijumaa
asubuhi kwa madai ya kuzungumza na wanafunzi na kutoa misaada, bila
mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa na taarifa.

Amesema, kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa na Serikali,yeyote
anayetaka kutoa misaada katika shule yeyote atoe taarifa kwa mkurugenzi
wa Halmashauri ili misaada hiyo ijulikane lengo lake na iweze kuratibiwa