Naibu waziri wa afya dr ndugulile ashangazwa na uchapa kazi wa wanawake ludewa

Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amewtaka
wanawake na vijana nchini kutumia changamoto zilizopo katika maneo yao
kama fursa ya kujiajiri na kuajiri watu wengine.


Dkt.
Ndugulile ameyasema hayo wilayani  Ludewa mkoani Nombe wakati
alipotembeela vikundi kazi vya wanawake na vijana vinavyojishughulisha
na kutengeneza barabara na madaraja madogo wilayani humo.

Dkt.Ndugulile
ameongeza kuwa vijana na wanawake wengi wamekuwa wakilalamika kukosa
ajira hasa kwa walimaliza elimu ya juu ila wanawake na vijana wa wilaya
ya Ludewa wamedhubutu kuchangamkia fursa ya kutengeneza barabara na
madaraja madogo.

“Sijawahi
kuona kitu kama hiki tangu nianze ziara zangu katika mikoa na wilaya
hongereni mmedhubutu na mkaamua ktuia fursa hii kupatakujiajir ni mwanzo
mzuri mtafika mbali” alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Ameogeza
kuwa jambo linalofanywa na vikundi hivyo linaendana moja kwa moja na
dhana ya Maendeleo ya Jamii  ya wananchi kushiriki katika shughuli za
kimaendeleo katika maneo  yao kwa kuamsha ari yao katika kushiriki
shughuli hizo pamoja na kujiongezea kipato.

Aidha
Dkt. Ndugulile amezitaka Hlmashauri nchini kuhimiza wanawake na vijana
kujiunga katika vikundi vya kijasiriamali ili kuwawesha  kupata mikopo
ya kufanya biashara na miradi mbalimbali kama wanavyofanya wanawake na
vijana wa wilaya ya Ludewa.

Dkt.
Nduguile amewapa moyo wanawake na vijana hao wa wilaya ya Ludewa katika
harakati za kutafuta kazi na kuwasihi vijana na wanawake wengine
kutojibweteka wakisubiri ajira za kujiajiri bali wajiongeze na kujiajiri
na hata kuajiri watu wengine.

“Jambo
hili mnalofanya ni jambo jema la msingi litawasaidia kupata kipato na
kujinua kiuchumi kwani kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  Mhe.Rais
Magufuli inasisitiza watu kufanya kazi hasa vijana na wanawake” alisema
Dkt. Ndugulile

Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha DARE Bi. Theopista Mhagama
amesema kuwa jumla ya vikundi 54 vimefanikiwa kujisajili katika Mamlaka
mbalimbali ambazo zitawawezesha kuomba na kupata kazi za kutengeneza
barabara na madaraja wilayani humo na Tanzania kwa ujumla

“Kwakweli
tunafarijika sana kwani tumeamua kwa dhati kujikwamua kiuchumi na sio
kukaa na kulalamika na kusbiri kufanyiwa kila kitu na Serikali wakati
kama vijana na wanawake tunaweza kufanya kazi tukajiajiri na kuajiri
wengine” alisema Bi. Theopista.

Ameongeza
kuwa mpaka sasa wamepata kandarasi ya kujenga madaraja madogo katika
barabara ya lwilo mbongo na yamefika katika asilimia 75 na wamedhutu
kuomba tenda za ujenzi wa barabara na madaraja  za kitaifa kwani
wanakidhi vigezo kama wakandarasi wengine.