Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lindi Jumbo Allan Mulligan kushoto alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma kwa mazungumzo ya kikazi. Kuliani Paul Shauri Meneja Mgodi wa Lindi Jumbo.
Na IssaMtuwa – Dodoma
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ametoa Baraka kwa Kampuni ya uchimbaji madini aina ya Graphite ya Lindi Jumbo iliyoko mkoani Lindi kuanza kazi ya ujenzi wa mitambo (Plant) na shuguli nyingine zinazohitajika ili kazi ya uzalishaji ianze.
Baraka hizo amezitoa leo tarehe 21/08/2019 ofisini kwake jijini Dodoma baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Lindi Jumbo Allan Mulligan aliyemtembelea kwa lengo la kumtaarifu kuhusu hatua iliyo fikiwa katika mchakato wa ujenzi wa mitambo, mabwawa ya maji taka, miundombinu mingine na uzalishaji.
Miongoni mwa mambo ambayo Mulligan amemweleza Naibu Waziri ni pamoja ukamilishaji wa ulipaji fidia kwa wananchi wa vijiji vya Namikulo, Matambarale Kusini na Namilema vilivyopo wilaya ya Ruangwa na kumweleza kwamba zoezi hilo limegharimu jumla ya kiasi cha Tsh. 4.6 bilioni, ambapo ulipaji ulifanyika kwa awamu tatu na hadi kufikia Agosti 21, fidia zote zimeshalipwa na hakuna mwananchi anayedai.
Aidha, Mulligan amemjulisha Naibu Waziri kuwa kwasasa kampuni husika inafanya matengenezo ya barabara na miundombinu mingine na ifikapo Oktoba 2019,ujenzi wa mitambo utanza na kwamba masharti yote ya kuzingatia yameshazingatiwa na kwamba wapo tayari kwaajili ya uzalishaji mara baada ya ujenzi wote wa miundombinu na plant kukamilika.
Kwa upande wake, Naibu Waziri amemshukuru mkurugenzi huyo wa Lindi Jumbo kutokana na kukamilisha suala la ulipaji wa fidia kwenye maeneo yote ya mgodi na ukamilishaji wa taratibu zote zinazohitajika kufuatwa kabla ya kuanza kwa uzalishaji ikiwemo ujenzi wa bwawa la majisumu (TFS).
“Nimefurahi kusikia taarifa hizi, hili mlilolifanya la kukamilisha ulipaji wa fidia ni jambo zuri sana, kwasababu hatupendi kuona migogoro kati ya mwekezaji na wananchi hasa katika masuala ya fidia kama ilivyotokea kwenye baadhi ya migodi, hongereni sana.”
“Sasa nendeni mkafanye hima kukamilisha miundombinu na ujenzi wa planti limuanze uzalishaji. Serikali inahitaji pesa kwa ajili ya wananchi wake ndio maana nahimiza mfanyeharaka kuanza uzalishaji ili serikali ipate mapato yake,”alisema Nyongo.
Mwezi Juni mwaka huu Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akiwa ameambatana na Kamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma walitembelea eneo hilo na kujionea shuguli mbalimbali za maandalizi ya eneo la ujenziwamitambo, eneo la bwawa la majisumu (TSF) na miundombinu ya makazi, hukumwakilishi wa Lindi Jumbo MenejawaMgodi, Paul Shauri akimweleza Mwenyekiti wa Tume ya Madini kampuni hiyo haina tatizo la fedha na kazi zote zinazo hitaji fedha hazitakwama na kwamba zitatekelezwa kwa wakati.