Pact tz yakutanisha asasi morogoro ktk mafunzo ya ufuatiliaji na tathmini ya miradi

Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, MOROGORO
SHIRIKA la Pact Tz kwa kushirikiana na shirika la Freedom House, chini ya mradi wa Data Driven Advocacy (DDA), imekutanisha maofisa miradi na maofisa ufuatiliaji na ufanyaji wa tathmini (Monitoring & Evaluation), ya miradi kutoka katika taasisi Zaidi ya 30 nchini Mkoani hapa kwa lengo la kuwafundisha namna bora ya ufuatiliaji wa miradi na kupata matokeo bora na sahihi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Afisa kutoka Pact Tanzania, Solomon Kibona amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha mashirika inayofanya nao kazi wanakuwa makini katika ukusanyaji wa takwimu katika miradi wanayoiomba.
Amesema kipengele cha takwimu hakipewi kipaumbele katika taasisi nyingi kutokana na dhana iliyojengeka miongoni mwao jambo limekuwa likisababisha kukosekana kwa matokeo mazuri kupitia miradi wanayoifadhili.

“Ubora wa takwimu ni muhimu sana kwa kuwa ndio linaloainisha matokeo sahihi, katika kila taasisi ijapokuwa ukweli ni kwamba taasisi zimekuwa zikiona suala hili halina umuhimu na limekuwa likigharimu fedha nyingi, “anasema.
Anasema katika mafunzo hayo washiriki wataelimisha kuhusu namna bora ya kukusanya takwimu kwa kuzingatia tatizo inalohitajika kufanyiwa utetezi, misingi ya kufuata na nyenzo zinazotakiwa kutumika katika kufuatilia miradi na kufanya tathmini.

Solomon Kibona kutoka Pact Tz akieleza dhana ya mabadiliko katika ufuatiliaji na tathmini ya miradi

Washiriki wa mafunzo ya M& E wakifuatilia kwa makini

Mkufunzi wa mafunzo ya M&E Olemari Mwenda akiwaelekeza washiriki wa mafunzo hayo namna ya kuhakikisha takwimu zinakuwa bora

Washiriki wa mafunzo ya M &E yanayoendelea mjini Morogoro wakimsikiliza mkufunzi kwa makini