Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mfuko wa hifadhi ya jamii PSSSF |
Wajumbe wa bodi pamoja na wafanyakazi wa mfuko wa hifadhi ya jamii PSSSF wakimpokea Waziri Profesa Ndalichako (hayupo pichani) alipokuwa akiingia ukumbini |
Menejimenti ya mfuko wa PSSSF walimsikiliza Waziri |
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF CPA Hosea Kashimba akizungumza kutambulisha wageni |
Wajumbe wa bodi na menejimenti walimsikiliza Waziri Ndalichako |
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi na wadhamini ya mfuko wa PSSSF, Mhandisi Mussa Iyombe akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri Profesa Ndalichako kumaliza kuzindua bodi ya mfuko huo |
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya mfuko wa PSSSF pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo |
*Ampongeza Mhe. Rais kwa
kuwezesha hatifungani kutolewa
*Asisitiza Uwekezaji uwe
wenye tija na endelevu,
Na Seif Mangwangi, Arusha
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Profesa
Joyce Ndalichako ameitaka bodi ya wakurugenzi ya mfuko wa Hifadhi ya Jamii PSSSF
kubuni na kuwekeza kwenye miradi yenye tija na uwezo wa kutengeneza ajira
nyingi pamoja na kuuingizia mfuko faida.
Pia
Waziri huyo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha kutolewa kwa hatifungani kama malipo ya deni
la Serikali kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Akizungumza
leo Ijumaa Machi 11,2022 alipokuwa akizindua bodi ya Wakurugenzi ya wadhamii ya
PSSSF iliyoteuliwa Disemba mwaka jana 2021. Waziri Ndalichako ameelekeza uwekezaji
uwe kwenye miradi yenye tija na endelevu na Mfuko uendelee kumuunga mkono
Mheshimiwa Rais kwa kuwekeza kwenye viwanda vyenye uhakika wa kuongeza ajira na
vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini.
“Nafahamu
mnawekeza katika viwanda, mfano kiwanda cha Karanga (kiwanda cha bidhaa za
ngozi cha Kilimanjaro), jana nilivaa viatu vya Karanga, ni vizuri sana,
nawapongeza sana. Kiwanda hiki kitasaidia sana wafugaji wetu kuuza ngozi”
alifafanua na kuongeza:,
“Tunamshukuru
sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya kipindi cha mwaka mmoja
amewezesha kutoa trilioni 2.17 kwa ajili ya kulipa deni hilo lililodumu kwa
muda mrefu.
Akizungumzia
kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi aliyoizindua, Profesa Ndalichako amesema
bodi hiyo inapaswa kushauri na kusimamia uwekezaji unaofanywa na Mfuko
kwa lengo la kulinda pesa za wanachama.
“Natoa rai kwa Bodi kuhakikisha mnatekeleza
majukumu yote. Nawapongeza kwa sababu Mfuko umeendelea kukua, naomba mhakikishe
masuala yote ya fedha mnayasimamia vizuri ili tuweze kulipa mafao. Naomba
mhakikishe mnawekeza kwenye miradi yenye tija”.
Kwa
upande wa watumishi wa PSSSF, Waziri Ndalichako
amewataka watumishi wa mfuko huo kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano ili
kufikia malengo yaliyopangwa.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba amesema katika
kuhakikisha lengo la kutoa huduma bora linatimia, mfuko umetekeleza mambo
mbalimbali ikiwemo kuboresha mtandao wa kiofisi kwa kila mkoa na baadhi ya Wilaya
zenye ofisi, kuanzisha kituo cha simu za bure kwaajili ya wanachama ambapo
huduma hutolewa hadi saa mbili usiku.
“uwepo
wa dawati la malalamiko ofisi zote za PSSSF, PSSSF kiganjani, kwaajili ya
wanachama kujihudumia wenyewe kwa simu, popote ulipo mtandaoni, uwepo wa anwani
pepe kwaajili ya kupokea hoja mbalimbali na uhakiki wa wastaafu kwa kutumia
alama za vidole,”amesema.
Akizungumzia
utendaji wa Mfuko CPA Kashimba, alisema tangu kuanzishwa kwake Mfuko
unatekeleza majukumu yake vyema chini ya usamimazi wa Bodi ya Wadhamini na
kuongeza kuwa changamoto zilizokuwa katika mifuko iliyounganishwa zimefanyiwa
kazi na sasa wanachama wa PSSSF wanapata huduma bora kwa kiasi kikubwa.
Wajumbe
wa Bodi ya Wadhamini iliyozinduliwa inajumuisha; Mhandisi Musa Iyombe (Mwenyekiti),
pamoja nae wajumbe wengine ni; Dkt. Aggrey K. Mlimuka, Bi. Suzan B. Kabogo, CPA
Stella E. Katende, Bw. Victor F. Kategere, Bi. Mazoea Mwera, Bw. Thomas C. Manjati, Bw. Said A.
Nzori na Bw. Rashid M. Mtima. Bodi ya Wadhamini ya PSSSF imeundwa kwa
kuzingatia utatu wa uwakilishi kutoka Serikalini, Wafanyakazi na Waajiri.
Akizungumza
baada ya uzinduzi wa bodi, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Iyombe amesema,
“Tunashukuru sana Mhe. Waziri kwa kuja kutufungulia, asante sana.
Nakuhakikishia kazi ya Bodi ni kukushauri, sisi kama Bodi tutatekeleza majukumu
yetu kwa uaminifu na uadilifu, tupo makini hatutakuangusha.
Hafla
ya uzinduzi wa Bodi ilihudhuriwa na; Profesa Jamal Adam Katundu, Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
ambaye ameitaka bosi hiyo kubwa mfano wa kuigwa dhidi ya bosi zingine kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa maadili.