Na Queen Lema Arusha
Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuboresha mazingira ya ufundi kutoka Katika vyuo mbalimbali hapa nchini kwani fani ya ufundi ni muhimu Sana Kwa maendeleo ya Teknolojia.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakati akifunga maonyesho ya NACTE VET yaliyofanyika katika viwanja vya shekh Amr Abeid mkoani Arusha
Alisema kuwa mpango huo wa Serikali unaenda sanjari na kugusa maeneo mbalimbali ya maendeleo ya vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na kuviboresha ipasavyo
“Elimu ya ufundi ni moja ya elimu ambayo ni muhimu sana na lengo halisi ni kuona kuwa elimu ya ufundi inapiga hatua ikiwa ni pamoja na kuzalisha mafundi wenye tija na kuepukana na ukosefu wa ajira kwani sekta binafsi inaweza kuajiri watu wengi zaidi”aliongeza
Aidha alitaja mikakati ya Serikali katika kuweza kumsaidia vyuo kuwa ni pamoja na kuanzia sasa kuweza kujenga vyuo vya Veta kwa kila wilaya zote hapa nchini
Alitaja mikakati mingine ni pamoja na kuimarisha vyuo vya maendeleo ya Jamii hapa nchini ambayo yanalenga kuweza kuongeza kiwango cha ajira
“NACT VET nayo ipo kwenye mikakati ya Serikali yetu kuweza kusaidia kuratibu mipango hiyo ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji Katika maeneo ya Sayansi,na Teknolojia kwani Hilo ni Agizo la Raisi kuwa kila wizara ijipange kuzalisha ajira na lengo ni kukuza uchumi wa nchi”aliongeza
Katika hatua nyingine alisema kuwa mpango huo wa vyuo bado haujaweza kuwaacha watu wenye ulemavu kwani nao Wana uwezo wa kuchangia maendeleo ya nchi.
“Ukiongelea maendeleo ya vyuo bado Napo tumegusa ambapo Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya Bilioni 2 na mpaka sasa tumeshafungua vyuo Zaidi ya 7″alisema
Alimalizia kwa kuvitaka vyuo mbalimbali kuendelea kubuni Aina ya Mafunzo ambayo yataweza kuwa chachu katika kuleta mabadiliko ya ajira hapa nchini.
Naye Katibu mtendaji kutoka NACT VET Dkt Adolf Rutayuga alisema kuwa wao kama Baraza wameweza kufanya maonesho ambayo yamehusisha vyuo mbalimbali lakini sasa ni vyema Kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanatembelea vyuo mbalimbali ili kupata maelekezo sanjari na elimu ambayo itawasaidia Katika kuleta mapinduzi kwenye sekta ya ajira
khanifa Jonas ni moja ya vijana ambao waliweza kutembelea maonesho hayo katika siku ya kufunga ambapo alisema kuwa NACT VET imeweza kuwafungua macho sana vijana hasa Wa kanda ya kaskazini kwa kuweza kuwaonesha fursa zilizopo kwenye vyuo
“Mimi natamani Sana kujua jinsi ya kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kuaminika na Leo nimejionea kutoka katika banda la Arusha Technical ambao pia ni chuo hapo sasa najipanga kujiunga na chuo hicho ila bila haya maonesho nisingeweza kujua au kutambua Hilo”alisema