Mkazi wa Arusha akipatiwa msaada wa kisheria, ikiwa ni moja ya shughuli za wiki nzima zinazoendelea jijini Arusha katika maadhimisho ya wiki ya Azaki |
Afisa Sheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Amani Mkwama akitoa jana ushauri kwa mmoja wa wananchi waliofika siko la Mbauda kupata ushauri wa kiaheria kwenye wiki ya Azaki. |
Na Cynthia Mwilolezi, ARUSHA
WADAU wa sheria mkoani Arusha, wameiomba serikali kuendelea na zoezi la urasimishaji ardhi, ili wananchi wawe na maeneo yanayotambulika kisheria na kuondoka na migogoro ya ardhi inayowasumbua.
Akizungumza jana jijini Arusha wakati akitoa msaada wa kisheria katika wiki ya Azaki,kwenye maeneo ya soko la Mbauda na Kilombero, Mratibu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Hamisi Mayombo alisema katika utoaji wao msada wa kisheria kwa Kanda ya Kaskazini wamebaini kesi nyingi ni za migogoro ya ardhi na masuala ya ajira.
“Kutokana na utitiri wa kesi hizi za ardhi sisi wadau wa sheria tunaomba serikali iendelee na zoezi la urasimishaji maeneo kwani maeneo ukipimwa itasaidia kupunguza migogoro hii,”alisema
Pia alishauri kuwe na mabaraza ya ardhi zaidi ya moja kwa wilaya zenye watu wengi kama Arusha na kwingine kuwepo moja kwa kila Wilaya ili kuharakisha mashauri ya kesi hizo.
Alisema kwa sasa changamoto katika kusuluhisha kesi hizo na zinalundikana kutokana na kuwa na baraza moja kwa Wilaya ya Arusha ambalo linahudumia Wilaya ya Longido,Monduli na kwingine.
Aidha alishauri serikali kuitazama upya sheria na sera za ardhi na urasimishaji ardhi na itungwe kulingana na matatizo yaliopo.
Mayombo alisema kwa upande wa ajira kesi nyingi zimetokana na janga la Uviko-19 ambapo waajiri wengi walishindwa Julia watumishi wao mishahara na kukatiza mikataba bila kufuata sheria.
“Sasa wengi wao hawaifahamu sheria hali hiyo akipata graduate utaratibu upi ili apate haki yake ndio maana sisi tumeona tutumie wiki hii ya Azaki kuwapa wananchi msaada wa kisheria,”alisema.
Ofisa Sheria kutoka LHRC,Amani Mkwama alisema katika msaada wa kisheria wanaoutoa wamebaini uwepo wa watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo wanaohitaji msaada wa mawakili mahakamani na baadhi kuandikishwa nyaraka za kisheria.
“Kila mmoja tunamsaidia kulingana na hitaji lake, hivyo tunawaomba wananchi kujitokeza kuja kupata msada huu bire hats wenye migogoro ya kifamiliya pia tunapokea na kuwapatia huduma stahili,”alisema
Mmoja wa wananchi waliopatiwa msada huo, Rashidi Msangi alishukuru LHRC na wadau wote wa sheria walionao kwani umesaidia tatizo aliloliwa nalo na sasa atafuta hatua alizoshauriwa.
Kituo cha sheria na Haki za Binadamu LHRC katika utoaji msaada huo wanasaidiana na Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA),Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Mfuko unaotoa msaada wa huduma za kisheria (LSF)