Na Jane Edward,Arusha
SPIKA wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Tulia Akson amesema kuwa ,Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wamekusanyika jijini Arusha kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo maswala ya kilimo.
Ameyasema hayo jijini Arusha kwenye kikao cha 53 cha jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinacholenga kujadili usalama wa chakula na tatizo la ajira kwa vijana.
“Hiki ni kikao cha 54 na ni mara ya nne kufanyika hapa nchini Tanzania kukusanya mabunge haya tunataka kuhakikisha Tanzania na jumuiya ya nchi za Afrika inajitosheleza kwa chakula.”amesema Dk.Tulia.
Amesema ,wanataka kuona vijana wengi wanajiwekeza katika eneo hilo na kuhakikisha wanajiajiri katika sekta hiyo ya kilimo kwani ni sekta ambayo inaajiri idadi kubwa ya watanzania .
Ameongeza kuwa, sasa hivi nchi ya Tanzania imeanza kupiga hatua na fedha nyingi zimewekezwa katika eneo hilo na wadau mbalimbali kujitokeza kuwekeza katika sekta hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha kuna uwekezaji wa kutosha katika sekta hiyo.
Amesema ,kwa sasa hivi Tanzania wanafanya vizuri sana na wanaweza kulisha Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.
Mkutano huo wa siku Saba unashirikisha wabunge wa SADC kutoka Zimbabwe,Namibia,Sherisheri,Afrika Kusini, Lesotho,Malawi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Eswatini,Angola, Botswana,Zambia, na wenyeji Tanzania.