Afisa Masoko Mwandamizi Tasac Martha Kelvin katika akimkabidhi zawadi kwa Naibu katibu mkuu wizara ya madini Msafiri Mbibo Mara baada ya kutembela kwenye banda la shirika hilo kwenye maonyesho ya Madini mkoani geita
WAKALA wa Meli Tanzania (TASAC) wamesema kuwa katika kutekeleza majukumu yao Shirika limejikita katika kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili kufahamu namna shirika hilo linavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.
Hayo yamesemwa Mkoani Geita kwenye maonyesho ya kitaifa yateknolojia ya madini na uwekezaji yaliyoanza Septemba 27 mwaka huu na Afisa Masoko Mwandamizi TASAC Martha Kelvin.
Martha amesema kuwa licha ya majukumu makubwa waliyonayo pia Shirika limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia maonyesho madini ili kufahamu namna linavyotekeleza kazi zake kama sheria inavyoelekeza.
“TASAC tunashiriki maonyesho haya ya tano ya madini hapa Geita ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya majukumu yanayotekezwa Kisheria.”ameseme
Amesema kuwa wao kama mdhibiti wa shughuli za usafiri wa maji wanasimamia huduma zinazotolewa na Bandari, wanadhibiti na kusimamia ulinzi, usalama na utunzaji wa mazingira na kuratibu shughuli za uokoaji na utafutaji pale panapotokea dhoruba katika vyombo vya usafiri kwa njia ya maji.
Pia ameongeza kuwa moja ya kazi wanayoifanya ni kutoa elimu kwa wananchi hususani mkoani humo wakiwamo wadau wa Madini katika jukumu lao la kipekee kwenye biashara ya Meli ambapo kwa sasa wanafanya uondoshaji wa shehena kwa makinikia na mashine zinazotumika katika migodi.
“Tunawakaribisha sana kwenye banda letu hapa kwenye mao nyesho mkoani geita ili kuweza kupata elimu zaidi itakayowasaidia kujua nini cha kufanya wanapotaka kuagiza mashine zao na kuziingiza hapa nchini na kuzitoa na usafirishaji wa Makinikia”amesema Martha
Amefafanua kuwa Kwa mujibu wa Sheria, TASAC ina wajibu wa kusimamia kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhimiza usimmizi na shughuli za uwakala wa meli wenye ufanisi, kuhimiza shughuli za bandari na huduma za meli zenye ufanisi, kuhakikisha kunakuwepo usalama na ulinzi wa shehena, kuhimiza na kutunza mazingira, usalama na ulinzi wa bahari, maziwa na mito.
Pia amesema Shirika hilo lina wajibu wa kuhimiza ufanisi, uchumi na uaminifu, kuendeleza upanuzi wa sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji, kuhimiza ushindani katika biashara ya uwakala wa meli, na kuingia kwenye majukumu ya kimkataba na watu wengine au kikundi cha watu.
Maonesho hayo ya tano ya Teknolojia ya uwekezaji wa Madini yana lengo la kuwaleta pamoja wadau mbalimbali katika Sekta hiyo na kubadilishana uzoefu wa kitaalamu na kujifunza Teknolojia za kisasa katika sekta hiyo pamoja na Taasisi zingine mbalimbali ikiwemo TASAC.