Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa Mshindi wa KWANZA katika kundi la Mamlaka ya Udhibiti wa Bidhaa na Huduma kwenye Maonesho ya 27 ya Wakulima Nane-Nane (08-08-2019) ki-Taifa yaliyo fanyika kwenye Viwanja vya Nyakabindi, Bariadi-SIMIYU. Pichani WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasimu Majaliwa akikabidhi Kombe la Ushindi kwa Mkuu wa TCRA- Kanda ya Ziwa Eng. Francis Mihayo Viwanjani hapo, Agosti 8,2019. (Picha na TCRA).
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yaibuka Mshindi wa Tatu Bora -kwenye kundi la Mamlaka za Huduma na Udhibiti-Sikukuu ya Wakulima Nane-Nane 2019 DODOMA. Pichani Mgeni Rasmi Dkt. Rehema Nchimbi(kulia) ambaye ni Mkuu wa Mkoa Singida, akimkabidhi Cheti, Mkuu wa TCRA- Kanda ya Kati Antonio Manyanda kwenye Uwanja wa Nzunguni Dodoma, wa Pili kulia ni Mkuu wa Mkoa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge. (Picha na TCRA).
KATIBU wa Baraza la Wazee, Mkoa DODOMA Alhaji-Mohammed Makbel(80) (kulia) na Mjumbe wa Baraza hilo Bi. Fatuma Mohammed Mtaki(79) kwenye picha ya Pamoja baada ya kusajili Laini zao za Simu kwa Alama ya Vidole -Viwanja vya Nane-Nane Jijini Dodoma, leo 7/08/2019. Wajumbe hao wa Baraza la Wazee Mkoa Dodoma wamehimiza Wananchi kusajili laini zao za Simu Kibiometria na Kuzingatia Matumizi Bora ya Mtandao.
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA Mhandisi Emelda Salum akiwa na Kikombe cha Ushindi wa Pili katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini.