Na Mwandishi Wetu.
Mwaka 2020 umekuwa mwaka wa changamoto karibu kwa kila mtu. Kwa kuwa sote tutasherehekea
moja ya vipindi bora vya mwaka, TECNO itakuwa ikifanya kitu tofauti mwaka huu kwa kuwapa kitu bora
mashabiki wao kwa kuongeza shauku na ujasiri katika mwaka mpya. Kwa kutumia hashtag za
“#HeadIntoTheNewYear” na “#CelebrateDifferent” pamoja na kushiriki kwenye kurasa rasmi za
mitandao ya kijamii za TECNO unapata nafasi ya kushinda zawadi kibao!
Ili kusherehekea kuelekea Mwaka Mpya, wafuasi wa Simu za Mkononi za TECNO watapata nafasi ya
kushinda zawadi nzuri wakati wowote ambapo Manchester City itacheza kwenye msimu huu wa
sikukuu.
Kwa kushirikiana na washirika wake Manchester City, TECNO inawataka mashabiki wanaoshiriki kote
Afrika Mashariki, Afrika Magharibi na Kusini Mashariki mwa Asia kuonyesha jinsi watakavyosherehekea
kitofauti msimu huu wa sikukuu na kuelekea Mwaka Mpya, hivyo kila wakati Manchester City
inapofunga bao au inaposhinda mchezo, wafuasi wa TECNO wanaweza kuonyesha furaha yako kwa
kutumia hashtag hizo na huwenda na wewe ukushinda pia!
Basi hebu tuonyeshe jinsi utakavyosherehekea magoli na ushindi wa Manchester City msimu huu wa
Sikukuu kwa njia yoyote unayotaka kuelezea. Inaweza kuwa video ya wewe na familia yako mkishangilia
nyumbani, picha ya wapi unatazama, au hata hadithi ya kwanini mchezo fulani una maana kubwa
kwako. Chaguo ni lako!
Mbali na zawadi zitakazo tolewa, video bora, hadithi, au picha zitaonyeshwa kwa baadhi ya wachezaji
wa Manchester City hapo Januari mwaka 2021, ambao ndio wataamua video, hadithi au picha bora –
kwa hivyo uwe mbunifu iwezekanavyo na maingizo yako ikiwa unataka kutambuliwa! Huwezi kujua,
unaweza kuwavutia tu na lolote linaweza kutokea!
Eric Mkomoye, Afisa Mahusiano TECNO alitoa maoni yake juu ya uzinduzi wa shindano hilo, "Ulimwengu
utakuwa ukisherehekea “kitofauti” katika kipindi hiki cha sikukuu, katika kila mwendo wa maisha na
haswa ndani ya mpira wa miguu. Kampeni yetu inamtaka kila mtu aingie mwaka mpya "kitofauti" kwa
kuchochea ubunifu na kuleta mshangao zaidi kwenye maisha. Tunataka mashabiki wetu kuchukua hatua
ya kuwa katikati kwa njia halisi inayohusiana moja kwa moja na ushirikiano wetu na Manchester City, na
kuonyesha msingi halisi wa kampuni ya TECNO na bidhaa zake. Kwa ufupi unaweza kusema, tunataka
kuhamasisha zaidi wateja wetu na kuwazawadia kwa kushiriki.”
Sio tu unaweza kushiriki mtandaoni, unaweza pia kushiriki katika maduka ya TECNO yaliyo chaguliwa na
yenye shughuli za mpira wa miguu ndani ya duka katika mikoa yote. Uliza tu rafiki au mfanyikazi wa
TECNO ukiwa ndani ya duka kukuchukulia filamu au picha ikionyesha unavyoshiriki kwenye moja ya
michezo yetu ya ' Head into the New Year’.
Tag TECNO Mobile ukitumia hashtag za #HeadIntoTheNewYear #CelebrateDifferent kwenye mitandao
ya kijamii ili kushinda. Zawadi za papo hapo zitapatikana dukani, na pia utaingizwa kwenye shindano kuu
ukituma picha yako kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa hivyo, toa simu yako na utuonyeshe jinsi utakavyokuwa ukielekea mwaka mpya kwa kusherehekea
msimu huu wa sherehe!
Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa huu – https://bit.ly/39XeDjb