Na Thabit Madai,Zanzibar.
WAFANYABIASHARA wadogo wadogo wakiwemo Mama lishe katika Soko la Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja wamemuomba Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwatatulia changamoto ya upatikanaji wa huduma ya choo pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.
Wafanyabiashara hao wamesema kwa muda mrefu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika eneo lao la kazi hivyo wamemuomba mgombea huyo endapo atachaguliwa kuwa rais wa Zanzibar kupitia chama chake aweze kuwatatulia changamoto hizo ambazo ni kero kwa kipindi kirefu.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti katika ziara ya Mgombea huyo ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake kwa kutembelea makundi mbalimbali ya wananchi katika maeneo yao husika.
Mauwa hassani hamza ni mama ntilie katika soko la kinyasini mfanyabiashara amesema kuwa shida kubwa ambayo kwa muda mrefu inawakabili ni kutokuwa na huduma ya choo pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama
Pia amesema katika eneo lao la biashara wanakosa sehemu ya kutupa taka na pamoja na kukosa mikopo ya kuwawezesha kujiinua kiuchumi.
Nae Mtumwa mkwaju amesema changamoto nyingine inayowakabili ni kuwepo kwa suala zima la udhalilishaji wa wanawake na watoto
Akizungumza na wafanyabiashara hao Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaahidi wafanyabiashara hao kuwajengea mfumo mzuri utakaowawezesha kupata fursa ya kukopeshwa mikopa na kuwainua kimaisha.
Dk. amesema suala la miundombinu ya soko atahakikisha linatatuliwa na kuwajengea soko la kisasa katika eneo hilo la kinyasini Wilaya ya Kaskazin ‘A’,Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Hata hivyo Mgombea huyo wa Urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kwamba iwapo atachaguliwa kuwa rais kwa haraka atatua kero ya unyanyasaji wa kijinsia na udhalilishaji wa wanawake na watoto visiwani humo.