Wakulima kaskazini wahimizwa kulima vanilla

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Wakulima kutoka katika kanda ya kaskazini wanatarajiwa kupewa mafunzo maalum kwa ajili ya kulima zao la Vanila ambalo ndilo zao la pili linalonauzwa kwa bei ghali duniani 

Mafunzo hayo ambayo yanaratibiwa na kampuni ya Vanila internationa limited Yanatarajiwa kufanyika January 28 mwaka huu Mkoani Arusha huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela 

Akiongea na vyombo vya habari mkurugenzi wa Kampuni ya Vanila Bw Saimon Mkondya  amesema kuwa wameamua kuleta elimu hiyo kwa kuwa zao hilo linaweza kuwasaidia jamii kuinuka 

Amesema tayari wameshafanya tafiti mbalimbali kwa mkoa wa Arusha na majibu ya tafiti hizo yameonyesha kuwa  Arusha zao hilo linaweza kustawi na  linastahimili Hali ya hewa iliyopo.

“Takwimu zinaonyesha kuwa endapo kama wakazi wa kanda hii wataweza kufanya kilimo hicho cha Vanila wataweza kupata fedha kubwa sana kwani Vanila ndio zao la pili lenye kuweza kuuzwa kwa bei kubwa Sana”aliongeza

Aliongeza kuwa Kampuni ya VANILLA INTERNATIONAL LIMITED bado imeendelea kuwasisitiza wananchi  kuwekeza katika kilimo cha vanilla kwani kilimo hicho ndicho kilimo pekee chenye uwezo mkubwa wa kukuinua kiuchumi.

Alibainisha kuwa  Zao la vanilla linaanza kuvunwa baada ya miezi 7(vikonyo) na mwaka 1 (matunda) lakini bado utahitajika kunavuna kwa miaka 60 tofauti na mazao ya Aina nyingine huku Kasi ya bei ikiwa ni kubwa Sana

Alihitimisha kwa kusema kuwa kwa Sasa Soko kubwa la zao la Vanila lipo Dubai na sehemu nyingine duniani kwani Vanila ni moja ya mazao ambayo yanatengeneza marashi,lishe, na pia kwa mujibu wa tafiti mbalimbali pia zao Hilo likitumika ipasavyo kwa Lina weza kuimarisha afya ya ajili

Naye Meneja wa kanda kutoka katika Kampuni hiyo ya Vanila Bi Miriamu Kessy alisema kuwa hiyo ni fursa pekee kwa vijana hususani kwa vijana wa kanda ya kaskazini kwa kuwa Vanila inalipa

Miriamu alisema kuwa uwekezaji wa zao la Vanila ni uwekezaji wa Kudumu na itaweza kunufaisha kizazi Hadi kizazi na kwa Sasa mtaji wa kuwekeza kwa zao Hilo ni wa gharama ambayo ni rafiki sana na jamii