Wakulima mbarali wapewa mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kilimo cha umwagiliaji


Mhandisi Karoli Lihala akijibu swali kutoka kwa katibu wa Skimu ya umwagiliaji Isenyela Bw. Samweli Ngeve wakati wa Mafunzo Chimala Wilayani Mbarali Leo.

Baadhi ya Wakulima katika picha wakisikiliza mada
 

Na Mwandishi Wetu, Chimala Mbarali

 

Wakulima katika Skimu ya
Isenyela wamepewa mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto
zinazowakabili katika kilimo cha umwagiliaji katika siku nyingine ya
mafunzo kwa wakulima hao.


Akitoa moja ya mada mhandisi Karoli Lihala kutoka Wilayani Mbarali
amewaeleza wakulima hao kuwa,ujenzi wa tuta katika njia ya kupeleka maji
mashambani ni njia nzuri ya kuimairisha sehemu ya juu ya mto.

Alisema kuwa, kusakafiwa kwa mifereji na kujengwa kwa makaravati kunaweza kuimarisha zaidi skimu hizo.

Aliongeza kwa kusema kuwa kabla ya miundombinu ya umwagiliaji
kuboreshwa na serikali “kwa sasa wakulima anaweza kuzingatia utunzaji wa
mazingira kwa kutoa mchanga katika mto, kulinda vyanzo vya maji, kutoa
magugu maji na kutofanya shughuli za kibinadamu kama kilimo katika
vyanzo vya maji.” Alisisitiza