Walimu watatu wauawa kwa shambulizi la kigaidi kenya

Watu watatu wameuawa baada ya wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab
kuvamia mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na
Somalia.
Walimu watatu ambao si wa eneo hilo walipigwa risasi hadi kufa huku
kituo cha polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa
katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.
Washambuliaji hao pia wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.
Maafisa wa polisi wanafuatilia wavamizi hao huku ripoti za kiusalama
zikionyesha kwamba wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika
barabara ya eneo hilo.
Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za
kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.
Wiki iliyopita, Uingereza imetoa onyo kwa raia wake wanaotaka kusafiri
nchini humo dhidi ya kutembelea kaunti ya Garissa na katika eneo la
ndani ya kilomita 60 katika mpaka wa Kenya na Somalia.
Hili ni shambulizi la 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya
katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi 4 yakitekelezwa Garissa, 3
Wajir, 2 Mandera na 2 Lamu.
Chanzo – BBC