Wanafunzi wadondoka darasani kwa kukosa njaa

Na Mwandishi Wetu, Arumeru

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya msingi Oldonyo Sambu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, wanadaiwa kudondoka darasani kutokana na kukaa na njaa kwa muda mrefu.

Mtendaji wa Kijiji cha Lemanda Bw. Gaspa Lembris amesema adha hiyo inatokana na Wananchi kushindwa kuwalipia watoto wao ili wapate chakula shuleni.

Aidha, Wananchi wamesema kutokana na badadiliko ya hali hewa kwa msimu  wa mwaka huu wa 2021 hawajapata mavuno yeyote mpaka sasa hivyo mbali na kushindwa kuwalipia watoto wao chakula shuleni pia wao binafsi wanaomba Serikali iweze kuwasaidia chakula kwakua wanakosa hadi mlo mmoja kwa siku. 

Pia, Mtendaji huyo ameieleza GADI TV kuwa mwanafunzi akidondoka anapewa soda na biskuti ndipo anapata nguvu, lakini wakati mwingine walimu hulazimika kwenda kuchukua chakula majumbani mwao na kuwapa pindi tatizo hilo linapotokea. 

“nimeshashuhudia watoto wanne na mara nyingi ni matukio yamekuwa yakitokea ndani ya wiki, ukweli ni kwamba pia kwa walimu imekuwa ni kazi kwasababu baada ya saa nne ufundishaji kwa walimu unakuwa ni mgumu kwa sababu watoto unakuta wameishiwa na wengine kutoroka” Mtendaji, Gaspa Lembris