Watu 30 wafikishwa mahakamani kwa uzururaji

Watuhumiwa wa kesi ya uzururaji wakipanda katika gari
ya polisi kuelekea katika mahakama ya mwanzo ya Nunge, iliyopo
Manispaa ya Morogoro
Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro limewafikisha mahakamani watuhumiwa 30 kwa makosa ya uzembe na uzururaji hususani katika kipindi cha usiku katika manispaa ya Morogoro.
 

Watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 16 mwaka huu katika eneo la Kahumba Manispaa ya Morogoro,eneo ambalo maarufu kwa biashara haramu za binaadamu huku baadhi ya wanaweke
hujihusisha na shughuli ya kuuza miili yao.
Watuhumiwa hao wakiwemo wanaweke 23 na wanaume 7 walikamatwa katika eneo hilo agosti 16 mwaka huu majira ya saa 6 usiku katika oparesheni iliyofanywa na jeshi la polisi wa doria
wakiongozwa na mkaguzi Copro Anold Njiro.
Aidha baada ya kufikashwa mahakamani watuhumiwa  wamesomewa mashitaka yanayowakabili na Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Nunge Emelia Mwambagi,ambapo amesema kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa makosa mawili ambayo ni uzembe na uzurulaji pasipo sababu.
Hata hivyo watuhumiwa wote wamekana mashitaka hayo na kesi hiyoitasomwa tene agosti 20 mwaka huu kutoka na kutokuwepo kwa mashahidi kwa upande wa mashitaka huku baadhi ya
watuhumiwa wakiachiwa kwa dhamana ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini bondi ya shilingi milioni moja.