WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu,akizungumza wakati
wa uzindua Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara
Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini
Dodoma,
Naibu Waziri Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),David Silinde
,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa pili wa miaka
mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla
iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma,
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Prof.Riziki Shemdoe ,akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala
wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti
12,2021 jijini Dodoma,
Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi
Victor Seff,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa pili wa
miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(TARURA) hafla
iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma,
Baadhi ya washiriki pamoja na viongozi
wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu,(hayupo pichani) wakati wa
uzindua Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara
Vijijini na Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini
Dodoma,
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu,akizindua rasmi
Mpango Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na
Mijini(TARURA) hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma,
…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amezindua Mpango
Mkakati wa pili wa miaka mitano wa Wakala wa Barabara Vijijini na
Mijini(TARURA) wenye thamani ya Sh.Trilioni 3.6.
Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti
12,2021 jijini Dodoma Waziri Ummy amesema kuwa Mpango huo unaanza mwaka
huu 2021/22 hadi 2025/26.
Mhe.Ummy ameeleza kuwa mpango huo
utaongeza mtandao wa barabara kutoka kilometa 2,404.90 hadi 3,855.65,
changarawe kutoka kilometa 29,116.57 hadi 102,358.14 na madaraja kutoka
2,812 hadi 6,620 na fedha zitakazotumika ni Sh.Trilioni 3.6.
“Mpango huu kwa miaka mitano unahitaji
Sh.Trilioni 3.6 sidhani kabisa Rais Samia kama atashindwa kwa kuwa
anauwezo wa kuzitafuta ndani ya miaka mitatu, twendeni tukaoneshe kazi
yenye ubora na ufanisi,”amesema.
Waziri Ummy amesema serikali
itaupatia Wakala huo magari 122 na mchakato wa kuomba ajira za Wahandisi
unaendelea na wataajiri Maofisa manunuzi kwa ajili na kutoa ajira za
muda.
Aidha Ummy, amesema kuwa kwenye miji
hiyo zitajengwa kilometa tano za barabara ya lami huku akisema kuna
andiko litaandaliwa kwa ajili ya miji ambayo haitapata.
Hata hivyo Ummy ametoa angalizo kwa
Wakala huo kuhakikisha kazi za ujenzi wa barabara zifanyike kwa ufanisi
kwa kuwa ni kipimo chao kwa watanzania.
“Tunataka tuone tija katika suala zima
la ukarabati wa barabara mijini na vijijini, ndugu zangu mnakazi kubwa
mwaka huu mmoja ndio mwaka wa kuwapima je, kile kisingizio cha kuwa
hamna fedha kilikuwa kisingizio au hamna uwezo na ubunifu na utashi wa
kazi mnazotakiwa kuzifanya,”amesema.
Amesema matarajio ya serikali kwa
Tarura ni makubwa sana hivyo wasiiangushe na waoneshe kuwa ni taasisi
sahihi ya kufungua barabara za mijini na vijijini.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi
hiyo, David Silinde, amesema TARURA katika historia ya nchi kwa mara ya
kwanza imetengewa fedha nyingi.
“Nipongeze Bunge kupitia kwa Spika
wetu Job Ndugai kwa kupitisha kiwango cha fedha, ambacho Tarura itaweza
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, malengo na mikakati tuliyojadili
hapa itatekelezwa kama ilivyokusudiwa,”amesema.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Prof.Riziki Shemdoe, amesema mkutano huo wa siku wa tatu
mbali na kuzindua kauli mbiu, watapitia utekelezaji wa Mkakati wa kwanza
wa miaka minne na kupitia Mkakati wa Pili wa mwaka 2021/22 hadi mwaka
2024/25.
Awali Mtendaji Mkuu wa TARURA,
Mhandisi Victor Seff ,amesema katika utekelezaji wa Mpango Mkakati
kuanzia mwaka 2017 hadi Juni mwaka 2021, jumla ya Sh. trilioni 1.3
zimetumika kutengeneza kilomita 24,979.24, ambapo kilomita 955.35
zimetengwa kwa kiwango cha lami, kilomita 16,857.82 za kiwango cha
changarawe.
”Madaraja 231 yamejengwa hivyo kuwa
na ongezeko la madaraja kutoka madaraja 2,960 hadi kufikia madaraja
3,191 na makaravati 1,325 yamejengwa hivyo kufikia makaravati 69,317
kutoka makaravati 67,992 ya awali”amesema Mhandisi Seff