Waziri wa kilimo josephat hasunga akutana waziri wa kilimo na waziri wa maendeleo vijijini wa israel

Na Mathias Canal, Bet Dagan-Israel

Waziri
wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 5 Septemba 2019
amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo
Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen na kukubaliana kwa kauli
moja kuwa serikali za nchi hizo mbili kuingia makubaliano ya kuendeleza
kilimo hususani katika utafiti, Tija katika uzalishaji, na Teknolojia.


Katika
mkutano huo uliohudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe
Job Daud Masima, Mhe Hasunga ametoa shukrani kwa Serikali ya Israeli
kuipatia Tanzania nafasi 100 za kujifunza kuhusu sekta ya kilimo kwa
vijana kupitia programu inayosimamiwa na Agrostudies.

Waziri
Hasunga ameeleza katika mkutano huo dhamira ya Serikali ya Tanzania
inayoongoza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John
Pombe Magufuli, ya kuwasaidia vijana waliorudi nyumbani baada ya mafunzo
hayo kwa kuanza kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo ardhi ambayo ipo
eneo litakalowawezesha kujiendeleza.

Vilevile
ameeleza kuwa katika wizara ya kilimo hakukuwa na kitengo cha masoko
hivyo ili kuwaunganisha vijana hao na masoko ya biashara watakazozalisha
serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Kilimo imeanzisha kitengo
maalumu cha kushughulikia masoko ya mazao mbalimbali ya wakulima.

Waziri
Hasunga pia amezungumzia kuhusu maeneo yanayoweza kuwavutia wawekezaji
kutoka Israeli ili kuwekeza nchini Tanzania kwa kutoa takwimu za ukubwa
wa ardhi yenye rutuba, uwepo wa maji na hali ya hewa inayoruhusu ukuaji
wa aina nyingi ya mazao.

Waziri
wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) amekutana na kufanya
mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri
Yehuda Ariel HaCohen, mkutano huo umefanyika Mjini Bet Dagan 
50250 nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa
Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen
wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la
Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.

Waziri
wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa
Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen
wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la
Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.

Serikali
ya Israeli ipo tayari kusaini hati ya makubaliano ya kilimo (Memorandum
Of Undarstanding-MOU) ya kilimo pale itapowasilishwa na Serikali ya
Tanzania, hii imekuja baada ya Mheshimiwa Waziri Hasunga kuona umuhimu
wa kuingia makubaliano ili iwe rahisi wawekezaji kutoka Israel kuzuru
Tanzania kuwekeza pamoja na kupata mikopo kutoka katika Serikali yao.

Akizungumza
kwa niaba ya Serikali ya Israeli Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini
wa nchi hiyo Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen imehaidi pindi Serikali ya
Tanzania itakapowasilisha mahitaji hasa kwenye mazao ambayo muhimu ya
kuanza nayo kwa ajili ya soko la Israel itakuwa tayari kushirikiana kwa
kutoa ujuzi pamoja na uwezeshaji wa wataalamu.

Hata
hivyo itakapotokea mwekezaji wa Israeli ataposhirikiana na kampuni ya
Tanzania, Serikali inawajibu kuingilia kati kusaidia maeneo ya
uwezeshaji na rasilimali watu.