Wilaya za wafugaji wasuasua chanjo ya uviko-19

 

Na Mwandishi wetu,Arusha

Mkoa wa Arusha , wilaya za wafugaji Mkoa wa Arusha zipo nyuma katika zoezi la kupata chanjo ya Uviko-19 hivyo sasa imepangwa kutumiwa viongozi wa Mila kuelimisha umuhimu wa chanjo

Mratibu wa chanjo ya Uviko-19 Mkoa Arusha Dk Willson Boniface amesema wilaya za Ngorongoro na Longido zipo nyuma katika chanjo awamu ya kwanza sasa mkazo wa umeongezwa katika elimu.

” Kulikuwa na upotoshwaji juu ya Chanjo Sasa Tumeanza kuboresha Utoaji elimu” amesema

Hata hivyo amesema Mkoa katika awamu ya kwanza uliofanya vizuri kwa kuchanja 47,950 kati ya Chanjo 50,000 zilizopokelewa.

 Mratibu wa chanjo ya Uviko-19 mkoa Arusha Dk Willson Boniface amesema zoezi la Chanjo awamu ya pili limeanza na wanatarajia Wakazi wengi kujitokeza.

Amesema katika awamu ya kwanza, Jiji la Arusha ndio limeongoza Kwa kuchanja watu wengi zaidi likifatiwa na Halmashauri ya Arusha Dc na Halmashauri ya Meru..

Amesema awamu ya kwanza jamii za kifugaji zilikuwa  nyuma kutokana  na upotoshwaji uliokuwepo lakini Sasa hali imeanza kuwa tofauti kutokana na elimu inayotolewa majumbani,Kwa viongozi wa Mila na makanisani.

Amesema Mkoa Arusha tayari umepokea chanjo nyingine 39,809 aina ya sinopharm ambazo mtu atapata chanjo Mara mbili.

“Baada ya kupokea chanjo za pili aina ya sinopharm Sasa elimu tunaendelea kutoa na watu wameendelea kuchanja”amesema

Amesema katika awamu ya pili watu watapata chanjo mara mbili tofauti na chanjo ya awamu ya kwanza ya Johnson & Johnson

” Tunaomba watu wajitokeze kwani chanjo zipo salama kabisa na safari hii chanjo itakuwa ni mara mbili”amesema.