Wizara ya mifugo yakabidhi vitendea kazi vya kisasa machinjio ya arusha

Kaimu katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi akipokea vifaa kutoka kwa Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji wizara ya mifugo Felix Nandonde kwenye makabidhiano yaliofanyika jana katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha na Pirsca libaga wa maelezo Arusha
Wizara ya mifugo na uvuvi imetoa vitendeakazi vya kisasa vya mazao ya mifugo kwa wachunaji wa ngozi kwenye machinjio yote ya mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongeza thamani na kuboresha uchunaji wa Ngozi.
Akikabidhi  vifaa hivyo leo,kwenye viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha  Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji wizara ya Mifugo na Uvuvi, Felix Nandonde amesema kuwa kwa kipindi kirefu ngozi zimekuwa  zikiharibiwa ubora wake wakati wa uchunaji kutokana na matumizi ya vifaa visivyo na ubora hivyo kupunguza thamani ya ngozi..
Amesema kuwa kabla ya leo kutolewa vifaa hivyo tayari wizara hiyo ilitoa mafunzo kwa wac vithunaji wote wa machinjio ya mifugo ya mkoa wa Arusha, mwaka 2019  mafunzo hayo yalikuwa ya  kuwajengea uwezo  wachunaji wa ngozi ili kuboresha thamani ya Ngozi.
Ndonde,amesema kuwa kwa kipindi kirefu sekta ya uchunaji ngozi kwenye machinjio ya mifugo,imekuwa inaonekana haina mwenyewe lakini sasa sekta hiyo inatambuliwa na kila mchunaji atapewa leseni, lengo ni kuongeza thamani ya mnyororo wa mazao ya mifugo nchini.
Ameitaja mikoa mingine itaayopokea vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Kilimanjaro,Manyara, Morogoro, Shinyanga,Kagera, Mwanza, Mara na Geita.
Alivitaja vitendea kazi hivyo kuwa visu vya kisasa ambavyo vimetengezwa kwa teknolojia ya kisasa na vimetolewa bure kwa wachunaji wa mkoa wa Arusha na pia vitatolewa bure kwa wachunaji wa mikoa mingine nchini.
 Akipokea vifaa hivyo kaimu katibu tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi, aliipongeza wizara hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wachunaji pamoja na vitendeakazi hivyo vya kisasa ambavyo vitawezesha kuongezeka kwa thamani ya ngozi mara baada ya kuchunywa kwenye machinjio.
Ameongeza kuwa vitendeakazi hivyo vitawezesha mkoa huo kuzalisha ngozi zenye ubora wa hali ya juu na hivyo ngozi zitakuwa na thamani kubwa na masoko ya hali ya Juu.
Amesema kuwa mkoa wa Arusha ambao ni wa wafugaji vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kusaidia kuondokana na matumizi ya vifaa butu ambavyo vilikuwa vikitumika kuharibu ubora wa Ngozi na hivyo kuondoa thamani yake.