Zaidi ya waongoza utalii 1000 wanatarajiwa kupatiwa elimu ya kuboresha utendaji kazi wao na kukabiliana na uviko-19.

Katibu wa chama Cha Waongoza watalii(TTGA)polinary kiwhili Akizungumza na Waongoza watalii kuwapa utaratibu wa mafunzo .

Na Mwandishi wetu,Arusha

Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza kutoa mafunzo kwa waongoza watalii 200  ili kuboresha utendaji kazi kipindi hiki  cha janga la Uviko-19 yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mafunzo hayo, yanayoratibiwa na  Chuo cha Usimamizi  Wanyamapori Mweka, yanaendelea katika hifadhi ya taifa ya Tarangire.

Mwenyekiti wa chama Cha waongoza watalii nchini(TTGA) Emmanuel Mollel mafunzo hayo ya siku 12 yanafaida kubwa kwao .

” tunapenda kuishukuru sana serikali na Wizara ya Maliasili na Utalii kuleta mafunzo haya”alisema

Mollel amesema mafunzo hayo ni Sehemu ya mpango wa maendeleo na Ustawi  wa taifa katika mapambano dhidi ya Uviko-19.

Hata hivyo aliomba washiriki wagharamiwe Kila kitu kama serikali ilivyoahidi kuliko Sasa kutakiwa kulipia chakula na malazi kwani bado waongoza Utalii wengi hawana fedha kutokana na athari za Uviko-19.

Kiongozi wa waongoza Utalii walioanza mafunzo,Max Mbise amesema wanamshukuru sana Rais Samia Suluhu kuwakumbuka kupata mafunzo kutokana na fedha za Uviko-19

Amesema katika mafunzo hayo watafundishwa kutoa huduma Bora Kwa watalii,kutoa huduma ya kwanza,maadili ya kuongoza watalii ,jinsi ya kukabiliana na Uviko-19 na elimu ya ndege na wanyama.