Zambia yakusudia kusajili mikokoteni yote

Mamlaka ya Zambia imepanga kusajili mikokoteni yote ambayo inatumika kwa matumizi ya kibiashara baada ongezeko la vitendo vya wizi.

Wasukuma mikokoteni husaidia kubeba mizigo mjini kwa gharama nafuu.Wafanyabiashara hupenda kutumia wachuuzi hao kwa sababu gharama ya usafirishaji wao ni nafuu.

Meya wa Lusaka bwana Miles Sampa alisema kumekuwa na ongezeko la malalamiko ya wizi kutoka kwa wafanyabiashara ambao hutafuta huduma hiyo .

Kutokana na malalamiko hayo ,meya ameamua kuanzisha malipo ya kodi ya mikokoteni hiyo.

“Baraza litasajili mikokoteni yote inayotumika kwa ajili ya biashara kwa sababu za kiusalama kutokana na ongezeko la malalamiko ya wizi katika masoko yetu.“Usajili wake utamaanisha kuwa watawajibika waziwazi kwa wale ambao wanafanya biashara sokoni na katika vituo vya daladala maeneo ya mjini,”alisema bwana Sampa na hakutakuwa na ushuru ambao wasukuma mikokoteni watatakiwa kulipa.

Wasukuma mikokoteni wameshauriwa kusajili mikokoteni yao katika shirikisho la wasukuma mikokoteni Zambia.#CHANZO BBC