*Ziara* *ya* *Kamati* *ya* *PIC* *Hifadhi ya Ngorongoro*
Picha za Matukio mbalimbali wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia masuala ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) kukagua utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Uwekezaji katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro tarehe 14 Machi, 2022
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) Mhe. Jerry Silaa (Katikati waliokaa), Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (wa kwanza kushoto waliokaa) na Naibu Kamishna wa NCAA (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii) Christopher Timbuka wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) wakati Kamati hiyo ilipotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kukagua utekelezaji wa miradi ya uwekezaji tarehe 14 Machi, 2022 |
|
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) Mhe. Jerry Silaa (Kulia), akisisitiza jambo wakati akiitimisha ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) walipotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kukagua utekelezaji wa miradi ya uwekezaji tarehe 14 Machi, 2022 |
|
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) Mhe. Jerry Silaa (Kushoto), wakati Kamati hiyo ilipotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kukagua utekelezaji wa miradi ya uwekezaji, Kulia ni Naibu Kamishna wa NCAA (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii) Christopher Timbuka |
|
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (kushoto) akiteta jambo na Naibu Kamishna wa NCAA (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii) Christopher Timbuka (Kulia)wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) ilipotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kukagua utekelezaji wa miradi ya uwekezaji, tarehe 14 Machi, 2022. |
|
Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (kulia) pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) wakipata maelezo mafupi kuhusu mradi wa ujenzi wa Barabara ya Seneto hadi Kreta ya Ngorongoro inayojengwa kwa kiwango cha tabaka gumu la mawe kutoka kwa Naibu Kamishna wa NCAA (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii) Christopher Timbuka (Kulia) wakati Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge (Uwekezaji wa Mitaji ya Umma) ilipotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kukagua utekelezaji wa miradi ya uwekezaji. |