Rose muhando afunguka yale yaliyojiri wakati akitolewa mapepo kanisani

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Rose Muhando hatimaye amezungumza kuhusu video iliyosambaa sana mitandaoni mnamo 2018.


Huku
watu wakiendelea kuwa na maswali kuhusu kudidimia kwake, video ya
msanii huyo akijibingirisha sakafuni akiwa amelala chali iliwaacha wengi
na hisia kinzani.

Akizungumza na SDE ya Kenya, Rose alikiri kwamba anafahamu fika kuwa tukio hilo lilitokea katika kanisa la Pasta Ng’ang’a.

Hata hivyo, hana ufahamu wowote wa namna alijipata katika kanisa hilo ama kile kilichojiri wakati alikuwa anaondolewa mapepo.

Mwimbaji
huyo anayesifika sana kwa wimbo Yesu Nibebe, pia alikanusha madai ya
kumuomba mchungaji huyo mwenye utata kumuombea uponyaji kama
ilivyobainika awali.

Muhando anaamini kuwa alifungwa macho kuingia katika kanisa hilo kwani alipoteza fahamu kipindi kizima cha maombi.

Rose pia alitambua kwamba Ng’ang’a alimpigia simu baada ya kufahamu alikuwa mgonjwa na akajitolea kumuombea.

Msanii huyo ambaye alikumbana na maumivu makali tumboni alikubali ombi la pasta huyo na kutembelea kanisa lake.

“Pasta
Ng’ang’a alinialika katika kanisa lake na niliwasili mapema siku moja.
Wakati wa kukombolewa, nilikuwa na maumivu makali tumboni na aliniambia
ataniombea. Nilizirai baada ya kusikia maneno yake matatu na hadi leo,
siwezi nikaelezea kile kilitokea,” alisema Rose.

Muhando,
kisha alikiri kwamba wanawe wana baba tofauti na wanaendelea vyema
popote walipo na pia wanaume walikuwa wamezoea kumwacha baada ya
kujifungua.

“Watoto
wangu wote wako shuleni. Wote wana baba tofauti kwa sababu wote
waliniacha wakati nilikuwa na mimba ama wakati mtoto alikuwa mchanga,”
alifunguka Rose.

Credit: Tuko Kenya