Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim
|

Hamis Juma (Katikati) Katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa
(kuliani kwake) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushotoni
kwake) Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. David Mrango
na viongozi wengine.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.
Ibrahim Hamis Juma (Katikati) Katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa
(kuliani kwake) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushotoni
kwake) Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. David
Mrangona viongozi wengine.

Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kufanya tathmini ya kazi
inayofanywa na wapelelezi pamoja na waendesha mashitaka katika kesi
iwapo wanatekeleza wajibu wao ipasavyo.

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhe. Joachim Wangabo alipomtembelea ofisini kwake akiwa katika
ziara ya kikazi mkoani humo, Jaji Mkuu alisema Mahakama ya Tanzania
inakabiliwa na changamoto ya kesi kutomalizika kwa wakati na wakati
mwingine haki kutotendeka kutokana na wapelelezi pamoja na waendesha
mashitaka kutotekeleza wajibu wao ipasavyo.

Aidha Jaji Mkuu ameishauri
Serikali kuwabana wapelelezi na waendesha mashitaka ili wawe wanajiandaa
vizuri katika kesi mbalimbali.

Alisema endapo kutakuwa na
maandalizi hafifu ya hati ya mashitaka katika kesi huweza kusababisha
upelelezi wa kesi hiyo kutofanyika inavyotakiwa na hivyo kupelekea
wakati mwingine haki kutotendeka na kusababisha mfumo wa sheria
kutoaminiwa na wananchi.

Alisema matumizi ya Tehama katika
kesi yatarahisha na kusaidia haki kutendeka na kesi kumalizika kwa
wakati huku akitolea mfano wa matumizi ya kipimo cha DNA kwenye kesi
kubwa kama vile za mauaji na ubakaji. Alisisitiza umuhimu wa hivyo
kuchukuliwa mapema kabla ya ushahidi haujapoa.

Akitolea mfano wa kesi kwenye
Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu alisema wakati mwingine Majaji hukutana na
changamoto ya maandalizi hafifu ya hati ya mashitaka kwa kuwa inakuwa
haiendani na tukio lenyewe.

Alisema kutokana na kukua kwa
sayansi na Teknolojia, hivi sasa wapelelezi hawana budi kuchukua
maungamo ya kesi kwa njia ya picha video. “Upelelezi bado uko karne ya
16 wakati wahalifu wako karne ya 21”, alisema Jaji Mkuu.

Kuhusu Mahakama kuanza kutoa
hukumu kwa lugha ya Kiswahili, Jaji Mkuu amesema suala hilo ni muhimu na
Mahakama italifanyia kazi. Aliongeza kuwa hivi sasa Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto kinatoa mafunzo kwa Mahakimu ya uandishi wa hukumu kwa
lugha nyepesi na inayoeleweka zaidi.

Awali akizungumza, Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa aliiomba Mahakama kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kesi
zinamalizika kwa wakati hususani zile zinazohusiana na mimba za utotoni
kwa wananfunzi wa shule za msingi pamoja na Sekondari zilizopo kwenye
mkoa wake.

Alisema tayari kesi 40 za makossa
hayo zimefikishwa mahakamani lakini kati ya hizo ni kesi tatu tu ambazo
zimesikilizwa na kutolewa maamuzi. Alisema katika kipindi cha mwaka moja
kanzia Julai 2018 mpaka Oktoba 2019 katika mkoa wake kuna jumla ya
wanafunzi 294 waliopata mimba wakiwemo 209 wa shule za sekondari na 85
wa shule za msingi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga
Mhe. Halfan Haule aliiomba Mahakama kuangalia uwezekano wa kuanza kutoa
hukumu kwa lugha ya kishwahili hasa kwenye ngazi ya Mahakama za wilaya
ili kuwawezesha wananchi kuzielewa kwa urahisi.

Alisema hivi sasa wananchi walio
wengi hutumia muda mwingi kuzunguka kwenye ofisi mbalimbali za
wanansheria ili kupewa tafsiri za hukumu zao hatua inayowafanya
kuchelewa kupata haki ikiwemo kuchelewa muda wa kukata rufaa endapo
wanakuwa hawajaridhishwa na hukumu zilizotolewa.

Jaji Mkuu ameanza ziara ya kikazi
Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga ambapo awali alikagua
miradi ya ujenzi katika mkoa wa Songwe pamoja na kupokea taarifa ya
utekelezaji ya Mahakama kuu kanda ya Sumbawanga. Jaji Mkuu anaendelea na
ziara kukagua shughuli za Mahakama katika wilaya za Nkasi na Kalambo.

Na Lydia Churi-Mahakama Sumbawanga