Alat yaipongeza manispaa ya kinondoni kwa kutekeleza miradi

Jumuiya
ya Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT) imeipongeza Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati
kwakutumia Local Fundi (Force Account).
Akizungumza
na watendaji wa Halmashauri hiyo mara baada ya kukamilisha ziara ya
kukagua miradi ya Halmashauri hiyo, Makamu Mwenyekiti wa ALAT , Stephano
Mhapa amesema kuwa Mkurugenzi Mtendaji Aron Kagurumjuli na timu yake
wamefanikisha kujenga miradi mikubwa ya maendeleo kwa kutumia mafundi wa
kawaida jambo ambalo limeonyesha nizamu ya matumizi mazuri ya fedha za
serikali.

Amefafanua
kuwa mradi wa Zahanati ya Mikoroshini iliyopo Kata ya Msasani imejengwa
kwa shilingi milioni 400.8 kwa kutumia mafundi wa kawaida wakati kwa
mkandarasi wakutangaza tenda ingetumia milioni 700 na kwamba Halmashauri
hiyo imeokoa kiasi cha shilingi milioni 300.
Aidha
Mhapa amesema kuwa“ ukiangalia Zahanati hii imekamilika vizuri na imara ,
tumejionea wenyewe, Mkurugenzi na timu yako tunakupongeza sana, na
halmashauri nyingine ziige mfano huu kutoka kwako, kazi ni kubwa
uliyoifanya lakini gharama yake ni ndogo, haya ni matumizi mazuri ya
fedha za serikali.”

Akizungumzia
mradi wa Soko la kisasa la Magomeni, linalojengwa kwa shilingi zaidi ya
bilioni 8.9 na Kituo cha Afya kilichopo Kigogo kinachojengwa kwa
shilingi milioni 700 , Mhapa amesisitiza kuwa Halmashauri ya Kinondoni
inapaswa kuigwa na Halmashauri nyingine kwa kazi kubwa wanayoifanya
sambamba na kuwa na matumizi mazuri ya serikali.

Halmashauri ya Kinondoni tangu mwaka 2015 imekuwa ikipata hati safi na
hiyo ni kutokana na kuwa na nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha za
serikali, hati safi inamanisha kwamba mnapokea pesa za serikali lakini
pia mnakusanya mapato ya ndani na kuyatumia vizuri” ameongeza.
Kuhusu
asilimia 10 ya fedha kwa ajili ya mikopo ya vijana , wakina mama na
walemavu,ambayo ni bilioni tatu, Katibu wa ALAT Elirehema Kaaya
ameipongeza Halmashauri kwakufanya vizuri kwani kiasi hicho cha fedha ni
sawa na bajeti nzima ya Halmashauri nyingine.
Kaaya
amesisistiza kuwa kazi anayoifanya Mkurugenzi Kagurumjuli ndio
inayotakiwa na Rais Dk. John Magufuli na hivyo kuagiza Halmashauri
nyingine ziige mfano wake.

Umefanya matumizi mazuri na sahihi ya fedha ambazo ni kodi za wananchi
wanyonge, kilichofanyika na Mkurugenzi mtedaji wa Kinondoni ni kwamba ,
Mhe. Rais Magufuli na Waziri wa Tamisemi Suleman Jafo wanasisitiza
kutumia local fundi (Force Account) ninashauri wakurugenzi wengine
wasikilize maagizo yanatotolewa na serikali.” Amesisitiza Kaaya.
Awali
akizungumza na viongozi wa ALAT, Mkurugenzi Mtendaji Kagurumjuli amesema
kuwa Halmashauri imefanikiwa kupata bilioni 32.8 kutoka Serikali kuu
kwa ajili ya ujenzi wa miradi mitatu ya kimkakati ambayo itaongeza
mapato kwa kiasi kikubwa.
Kagurumjuli
alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzo wa soko la kisasa la Magomeni, wenye
thamani ya shilingi bilioni 8.9, ujenzi wa soko la kisasa la Tandale
wenye thamani ya shilingi bilioni 8.7 na uboreshaji wa fukwe ya Osterbay
(Coco Beach) wenye gharama ya shilingi bilioni 13.
Muonekano wa ndani wa soko la kisasa la Magomeni .
Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Ndugu Aron
Kagurumjuli, akiwa na wajumbe wa kamati ya ALAT Taifa , wakikagua
Zahanati ya Mikoroshini iliyopo kata ya Msasani, katika ziara ya
viongozi wa ALAT waliyokuwa wakikagua miradi ya Halmashauri hiyo jana.
Wajumbe
wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania ( ALAT) wakiangalia jengo la
soko la kisasa la Magomeni inalojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni
8.9.
Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni , Ndugu Aron
Kagurumjuli mwenye suti ya dakbluu, akiwaonyesha Makamu Mwenyekiti wa
ALAT Stephano Mhapa mwenyeshati la madoa akiwaonyesha mazingira ya
Zahanati ya Mikoroshini iliyopo Kata ya Msasani.