Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akisalimiana na Meneja Miradi wa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ Mkoani Kilimanjaro, Bw. Charles Shang’a alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi kwa ajili ya hafla fupi ya kupokea Misaada ya Kibinadamu iliyotolewa na Asasi hiyo kwa ajili ya wafungwa leo Novemba 15, 2019 |
.
Meza kuu wakiongozwa na Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike (wa pili toka
kushoto) wakiimba wimbo wa Taifa la Tanzania ikiashiria ufunguzi wa
hafla fupi ya kupokea misaada ya Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa
iliyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life In Christ. Tukio hilo
limefanyika leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu Karanga
Moshi.

Kaimu Mkurugenzi wa Asasi ya
Dorcas Aid International Tanzania Bw. Joseph Kumwembe akitoa maelezo
mafupi kabla ya kukabidhi msaada wa Kibinadamu kwa ajili ya Wafungwa
nchini. Dorcas Aid International Tanzania hushirikiana na Asasi ya
Kidini ya New Life In Christ katika kutoa misaada ya namna hiyo.

Kamishna Jenerali wa
Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike akitoa hotuba kwa wageni
mbalimbali (hawapo pichani) waliohudhuria hafla fupi ya kupokea msaada
wa Kibinadamu kwa ajili ya wafungwa kutoka kwa Asasi ya Kidini ya New
Life In Christ leo Novemba 15, 2019 katika viwanja vya Gereza Kuu
Karanga Moshi.

Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, CGP – Phaustine Kasike akipokea msaada wa baiskeri ya walevu
pamoja na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Asasi ya Kidini ya New Life
In Christ leo Novemba 15, 2019 kwa ajili ya wafungwa. Hafla ya upokeaji
wa misaada hiyo imefanyika katika gereza Kuu Karanga Moshi.

Muonekano wa baadhi ya misaada ya
Kibinadamu iliyotolewa Asasi ya Kidini ya New Life In Christ
iliyokabidhiwa kwa Jeshi la Magereza leo Novemba 15, 2019 katika viwanja
vya Gereza Kuu Karanga Moshi. Misaada imekabidhiwa leo kwa ujumla wake
ina thamani ya zaidi ya milioni 183.

Mhandisi ujenzi wa Jeshi la
Magereza, SP. Julius Sukambi akitoa maelezo ya kitaalam kwa Kamishna
Jenerali wa Magerezanchini, CGP – Phaustine Kasike alipotembelea katika
eneo hilo la ujenzi wa Kiwanda Kipya cha bidhaa za ngozi kinachojengwa
nje ya eneo la Gereza Kuu Karanga, Moshi

(Picha zote na Jeshi la Magereza).
…………………..
Na ASP Lucas Mboje, Moshi
ASASI ya Kidini ya New Life In
Christ imekabidhi kwa Jeshi la Magereza misaada ya vitu mbalimbali yenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni 183 ambayo itawanufaisha wafungwa
na Mahabusu waliopo magerezani katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na
Tanga.

Akizungumza kabla ya kukabidhi
misaada hiyo ya wahalifu waliopo magerezani, Kaimu Mkurugenzi wa Asasi
ya Dorcas Aid International Tanzania, Bw. Joseph Kumwembe amesema vifaa
vilivyokabidhiwa ni magodoro, sabuni, nguo za watoto, mabranketi,
vipeperushi, vifaa vya usafi na vitabu vya kiroho.

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ameishukru Asasi hiyo isiyo ya
Kiserikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kutekeleza kwa ukamilifu utoaji wa misaada ya kibinadamu pamoja na
baadhi ya huduma muhimu kwa wafungwa ikiwemo mafunzo ya Kijasiriamali
kwa wafungwa hivyo kulisaidia Jeshi la Magereza katika suala zima la
urekebishaji wa wafungwa.

“Niwashukru sana Asasi hii kwa
moyo wao wa upendo na kujitolea na niwapongeze sana kwa kutambua kwamba
wahalifu waliopo magerezani ni Binadamu kama walivyo Binadamu wengine na
wanahitaji misaada ya ki-binadamu kama hii,” Amesema Jenerali Kasike.

Aidha, Jenerali Kasike ametoa wito
kwa Asasi nyingine zisizo za Kiserikali kuiga mfano uliooneshwa na New
Life in Christ na Dorcas Aid International Tanzania ili ziweze
kushirikiana na Jeshi la Magereza kwa manufaa ya Taifa.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike amewataka Wakuu
wote wa Magereza yaliyonufaika na misaada hiyo kuhakisha kuwa misaada
inawanufaisha walengwa kwa maeneo yaliyokusudiwa samabamba na kusimamia
vyema vifaa hivyo.
Kamishna Jenerali wa Magereza
nchini, Phaustine Kasike mara baada ya kupokea misaada hiyo ametembelea
eneo la mradi mkubwa wa uwekezaji wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi
ambacho ni cha ubia kati ya Jeshi la Magereza pamoja na Mfuko wa hifadhi
ya jamii wa PSSSF. Kiwanda hicho kinajengwa katika eneo lililopo nje ya
Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo amewasisitiza wakandarasi wa ujenzi
huo kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.