Aweso awataka wenyeviti wapya wa vijiji,vitongoji wasigeuke kuwa wauza ardhi badala yake wawatumikie wananchi

 MBUNGE
wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso na Naibu Waziri wa Maji
akizungumza  na wananchi Kata ya Kipumbwi wilayani humo ambapo aliwataka
wevyeviti wapya kuhakikisha wanachochea kasi ya maendeleo kwa wananchi
wa

 MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza 

 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia akizungumza kushoto  ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah

 KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza

 MBUNGE
wa Jimbo Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji 
katika akikata utepe kushiria ufunguzi wa tawi la kikoba la Jipe Moyo la
Pangani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Pangani Rajabu Abdallah

 MBUNGE
wa Jimbo Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji
akicheza pamoja na wenyeviti wapya waliopita wilayani Pangani kwenye
uchaguzi wa serikali za mitaa

 Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji

MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso amewataka wenyeviti
wa Vijiji, vitongoji na mitaa waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za
mitaa uliopita wasiwe chanzo cha migogoro kwa wananchi kwa kugeuka wauza ardhi
bali wahakikishe wanashirikiana nao kutatua kero zinazowakabili.
Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji aliyasema  wakati mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani
ambapo alisema lazima watambue dhamana kubwa walioibeba ni kuhakikisha wanakuwa
mstari wa mbele kuchochea maendeleo kwenye maeneo yao.
Alisema kwamba wananchi wanataka maendeleo ndio maana
wamewachagua hivyo wanajukumu kubwa la kutekeleza hayo kwa vitendo ikiwemo
kutetea maslahi yao pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
“Unapokuwa kiongozi lazima utetee maslahi ya wananchi
wako pia utembue changamoto zinazowakabili hapa kipoumbwi asilimia kubwa wananchi
shughuli zao na uvuvi hivyo Mwenyeviti mpya wa hapa kuwa imara kusimamia wavuvi
waweze kuvua kwa usalama wapate ridhiki yao ya halali”Alisema Aweso.
Mbunge huyo pia aliwaambie wananchi kwamba hakuna
demokrasia yoyote ya kutafuta viongozi kwenye Taifa hili zaidi ya uchaguzi
hivyo vikiwemo kuwataka iongozi ambao wamepatikana watambue kwamba wana
kipumbwi na wana Pangani wanahitaji maendeleo na sio jambo jingine.
Hata hivyo pia aliwataka pia hakikisha kila baada ya
miezi mitatu wanasoma mapato na matumizi huku akiwaambia kwamba sio wakati
ukiwa umefika hata simu zao hazipatikani kwa kuwaeleza huo utakuwa sio
uoingozi.
“Wapo watu wamewaaminisha watu kwamba CCM ikiingia hapa
Kipumbwi watateseka hawataleta maendeleo…lakini wapo watu wanasema baada ya CCM
kuingia hapa eti boti zitafukuzwa hafukuzwi mtu hapa “Alisema Mbunge huyo.
Mbunge huyo aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa
bidii ili kuweza kuwapa maendeleo wananchi hao maana hawana wenyeviuti wengine
zaidi ya nyie.

“Eneo la Kipumbwi ni eneo lenye mapato makubwa watu
wanataka kupata maendeleo leo sizije fedha zinakusanywa nyingi lakini hata choo
 cha kujisaidia hakuna hakikisheni
mnabadika sasa”Alisema