Bakiza kuandaa kanuni zitakazosimamia haki za waandishi

Katibu
mtendaji wa Baraza la kiswahili BAKIZA Dkt.Mwanahija Juma akizungumza
na washiriki wa Kongamano la tatu la Kiswahili la Kimataifa
lililofanyika Zanzibar

Na.Vero Ignatus,Zanzibar.
Baraza
la kiswahili la Zanzibar (BAKIZA )imeandaa kanuni zitakazosimamia haki
za waandishi kwa kukusanya mirabaha kutoka kwa taasisi za elimu
mashirika ili kulinda kazi za waandishi.

Hayo
yamebainishwa kwenye kongamano la tatu la kiswahili kwa siku mbili na
kuwakutanisha washiriki 270 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Akizungumza
Katibu mtendaji wa Baraza la kiswahili (BAKIZA) Dkt.Mwanahija Juma
amesema kuwa washiriki wa kongamano la pili waliwashauri BAKITA na
BAKIZA kuwaenzi waandishi wakongwe na kuhamasisha waandishi chipukizi
kuandika kazi mbalimbali za kiswahili.

Amesema
katika kuadhimisha siku ya kiswahili duniani kila mwaka wamekuwa
wakihamasisha waandishi chipukizi kwa kuwafanyia mashindano na kuwapa
mafunzo 

Mwaka huu machi ,2019 walitoa mafunzo ya hadithi fupifupi kwa waandishi walioshiriki mashindano ya hadithi fupi”

Aidha
walitoa azimio la kuwataka Bakiza litoe ithibati kwa vitabu
vinavyochapishwa hivyo wametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wote wa
vitabu wa zanzibar wasichapishe vitabu kabla ya kuvipitisha Bakiza ili
kuvipa ithibati.

Amesema
kuwa washiriki walitoa azimio la kuandaa ziara ya utalii wa Kifasihi
jambo ambalo limefanyiwa kazi katika kongamano la tatu la mwaka 

“Tumeandaa
ziara katika mitaa aliyoitaja mwandishi Shafi Adam Shafi katika kitabu
cha Kuli iliwemo Bansatini ,Malindi,Darajani ,Msikitimabuluu,Gulioni,Kwahajitumbo,Kibiritingoma na Makaburimsafa.

Hivyo
BAKIZA wameiomba Taasisi ya Hakimiliki iangalie upya mirabaha ya
waandishi wa habari wanayopewa kutoka wauzaji wa vitabu na wachapishaji.