KAIMU Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire kulia akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe wakati alipotembelea Banda lao
KAIMU Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa maonyesho hayo.
KAIMU Meneja
wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire amesema watatumia maonyesho ya 8 ya
biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga ili
kuelezea huduma wanazozitoa kwa wananchi kwa sababu lango la bandari ni
kurahisisha biashara.
Ngaire
aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda
lao ambapo alisema wanarahisisha biashara kwa kupakua mizigo inayoingia
na kupakia inayosafirishwa nje hivyo huduma zao zinaathiri moja kwa moja
maisha ya wananchi zinapokuwa bora zile bidha zinazopakulia mwisho
gharama zikiwa kubwa za Bandari zinakwenda kuwaathiri wananchi.
Alisema
kwenye maonyesho hayo watawaeleza kwamba bandari ya Tanga inafanya nini
katika kurahisisha biashara na watawaeleza wananchi wa Tanga Bandari
inafanya nini katika kurahiisisha biashara na kuongeza thamani ya ubora
wa huduma.
Alisema ubora
wa huduma ambazo zinatolewa lazima kuwe na vitendea kazi vya kutosha na
bora kwa kuhakikisha meli inapokuja Bandarini lazima ikae muda mfupi
kwa sababu ikikaa muda mrefu inaonyesha kwamba hiyo Bandari haina
ufanisi.
Alisema
kipimo cha Bandari yoyote Duniani ni ufanisi na kiasi gani mzigo
unapakulia kwa saa na kiasi gani cha muda unamuhudumia mteja anapokuja
kufuata huduma bandarini.
“Lakini unaweza
kushindwa kutoa huduma bora kama vifaa ulivyonavyo vinaharibika mara
kwa mara na hivyo kujikuta ukishindwa kufikia malengo
uliojiwekea”Alisema
Hata hivyo
alisema katika mwaka uliopita 2019/2020 walihudumia tani 569270 za
shehena na mwaka huu ndani ya miezi sita wamehudumia tani 349205 na hivi
sasa wameanza kupata shehena inayosafirishwa kwenda nchi jirani
inayotumika kutengeneza saruji.