Benki
Kuu ya Tanzania imezitoza faini benki tano za biashara kwa kukiuka
kanuni namba 17, 22 na 28 za Kanuni za Kuzuia Utakatishwaji wa Fedha
Haramu za mwaka 2012 kwa kushindwa kuhakiki taarifa za utambulisho wa
wateja na kushindwa kuwasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka
katika Kitengo cha Kuzuia Fedha Haramu (FIU). Benki hizo na kiasi cha
faini ni kama ifuatavyo:
1.African Banking Corporation (T) Limited TSH 145 milioni 2. Equity Bank (Tanzania) Limited TSH 580 milioni
Pamoja na faini hizo, Benki Kuu ya Tanzania imezitaka benki hizo
kutekeleza yafuatayo ndani ya kipindi cha miezi mitatu toka tarehe faini
zilipotozwa:
- Kupitia
upya taarifa za wateja wao na kuhakikisha kwamba zinakidhi matakwa ya
kisheria na kanuni zilizopo za uhakiki wa utambulisho wa wateja (KYC); - Kuwasilisha taarifa ya miamala yenye kuleta mashaka ambayo ilitakiwa kuwasilishwa FIU;
- Kufanya
tathmini ya ubora wa mifumo ya ndani ya kibenki na kuchukua hatua
stahiki kuhakikisha kuwa mifumo hiyo ipo madhubuti kwa lengo la kukinga
mapungufu hayo hayarudii tena; na - Kuwachukulia
hatua stahili za kinidhamu, wafanyakazi wote waliohusika kufanikisha
ufunguaji wa akaunti za amana kinyume na kanuni za kumtambua mteja
(KYC).
Benki
Kuu ya Tanzania inapenda kuzikumbusha benki na taasisi za fedha
kuhakikisha kuwa zinafuata sheria na kanuni zilizopo nyakati zote.
BENKI KUU YA TANZANIA
botcommunications@bot.go.tz
19 SEPTEMBA 2019