Bilioni 943 zatumika elimu bila malipo

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, William Ole Nasha,akizungumza na wakati akifunga mkutano
mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu shule za msingi Tanzania
bara uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya
Msingi kutoka TAMISEMI Dr.George Jidamva,akitoa taarifa wakati wa
kufunga mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu shule za
msingi Tanzania bara uliofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa walimu
(Tapsha) ambaye pia ni Mwalimu wa Makuburi Jeshini Ubongo jijini Dar es
Salaam Bi.Rehema Ramole,akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa
Wenyeviti wa walimu wakuu shule za msingi Tanzania bara uliofanyika
jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Mwenezi wa Umoja wa
walimu (Tapsha) Mwl Odas Bambaza akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi
ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William
Ole Nasha,wakati wa kufunga mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa
walimu wakuu shule za msingi Tanzania bara uliofanyika jijini Dodoma.
Sehemu
ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu
shule za msingi Tanzania bara uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, William Ole Nasha,akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
washiriki wa Mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu shule
za msingi Tanzania bara uliofanyika jijini Dodoma.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI imesema katika kipindi
cha miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli kiasi cha Sh.Bilioni
943 zimetumika kwa ajili ya mpango wa elimu bila malipo.
Kauli hiyo aliitoa jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha wakati
akifunga mkutano mkuu wa kwanza wa wenyeviti wa walimu wakuu shule za
msingi Tanzania bara.
” Katika kipindi hicho kumekuwa na
mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu ambayo yamechochewa na mambo
mbalimbali ikiwemo mpango wa elimu bure na ujenzi wa miundombinu.
“Kwa miaka minne sasa serikali
inatekeleza mpango wa elimu bila malipo ambapo Sh.bil.24 zinatolewa kwa
mwezi, na Sh.bil. 943 zimeshatumika tangu serikali ya awamu ya tano
iingie madarakani.
Alisema kuwa wanaopelekewa fedha
kusimamia ni walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari, hivyo
isingekuwa wao kuwa wasimamizi wazuri wasingepata mafanikio makubwa.
Wakati huohuo alisema kwa kipindi
hicho nchi imepiga hatua kubwa katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu
ya shule za msingi na sekondari ili kuwa na mazingira mazuri ya
kufundishia na kujifunzia.
“Kuanzia mwaka 2016 hadi sasa
zimetumika Sh.Bilioni 308 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu kwa shule
za sekondari na msingi, wasimamizi wakuu wa miundombinu hiyo katika
ujenzi wake,”alisema.
Pia alisema kwa kipindi hicho viwango vya ufaulu vimekuwa vikipanda bila kushuka.
“Matokeo ya darasa la saba mwaka
2016 ufaulu ulikuwa wa jumla asilimia 70.2 huku mwaka 2017 ulipanda na
kuwa asilimia 72.8, mwaka jana(2018) imefikia asilimia 77.72 na sifa
hizi zinakuja kwenu walimu kwa kushirikiana na wazazi kw kuongeza
ufaulu,”alisema.
Hata hivyo, alisema kwa upande wa
kidato cha nne wastani wa ufaulu kwa mwaka 2016 ilikuwa asilimia 70.4,
pia mwaka 2017 ni asilimia 77.6 huku mwaka  2018 ni asilimia 78.4.
Alisema kuanzia mwaka 2016 hadi sasa serikali imeshatoa Sh.Trilioni 1.8 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu.
Ole Nasha alisema serikali inaendelea kushughulikia tatizo la upungufu wa walimu.
“Ombi la walimu wakuu kupatiwa
pikipiki naomba nilibebe ni suala la kibajeti, ni kweli mngeweza
kusaidia mafanikio makubwa ,”alisema.
Naibu Waziri huyo alisema serikali inajipanga kupitia sera ya elimu ili kuendana na mifumo ya ufundishaji ya karne ya 21.
Awali  Mwenyekiti wa Umoja wa
walimu hao(Tapsha),Rehema Ramole alisema siku mbili za mkutano huo
wamepata mafunzo mbalimbali ya uongozi, haki na wajibu wao na
kukabiliana na rushwa.
“Naomba walimu wakuu hao wapatiwe pikipiki ili kurahisisha usafiri kutokana na kufanya kazi kwenye mazingira magumu”alisema.