Na Mwandishi Wetu, APC BLOG DSM
Rais Magufuli leo Novemba 3, 2019 amemteua Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Uteuzi huo unaanza kesho, Kichere anachukua nafasi ya Profesa Mussa
Assad ambaye kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano kinaishia kesho.
Assad ambaye kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano kinaishia kesho.
Mteule huyo ambaye alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli ambaye alimteua tena kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, mwaka huu.
alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli ambaye alimteua tena kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, mwaka huu.
Akisoma taarifa ya uteuzi huo leo Jumapili Novemba 3, 2019, Balozi John
Kijazi amesema nafasi ya Kichere itajazwa na Katarina Revocati ambaye
alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
Kijazi amesema nafasi ya Kichere itajazwa na Katarina Revocati ambaye
alikuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
Pia, Rais Magufuli amewateua Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Kuwait, Kanali Francis Mbindi kuwa kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu
na majaji 12 wa Mahakama Kuu.
Kuwait, Kanali Francis Mbindi kuwa kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu
na majaji 12 wa Mahakama Kuu.