Breaking : sumaye ajiondoa chadema

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fredrick Sumaye leo Desemba 4, 2019 ametangaza kuondoka Chadema.

Akiongea leo kwenye mkutano wake na
waandishi wa Habari, Sumaye amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na
figisu alizofanyiwa baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya
Mwenyekiti wa Chadema Taifa. 


Ameeleza kuwa alitaka kugombea nafasi ya
Uenyekiti ili kuondoa dhana iliyopo miongoni mwa watu kuwa nafasi ya
Mwenyekiti ndani ya CHADEMA ni ya Freeman Mbowe na haiguswi. 

Amesema baada ya kutafakari kwa kina na kuona wakubwa wamewashawishi watu wa Kanda ya Pwani kumpigia kura ya Hapana.

Pia ametaja sababu za kusitisha nia ya
kugombea Uenyekiti wa Chama Taifa. ‘Nasitisha rasmi safari hiyo kwa
usalama wangu, usalama wa wanachama na chama chenyewe, maana Mwenyekiti
Mbowe ameshasema sumu haionjwi kwa ulimi na mimi sitaki kuionja kwa sumu
hiyo. 

Ametangaza kuwa hajiungi na chama chohote ila yupo tayari kutoa ushauri kwa chama chochote hata CHADEMA akihitajika.

Hapo chini kuna nukuu ya mambo aliyoyasema leo;

“Lile tangazo lililotoka jana, ilikuwa
ni kweli kutoka kwenye Ofisi yangu lakini halikutengenezwa kwa lengo
lile kwa hiyo naomba mliache kama lilivyo.

“Najua kuna mambo mengi yameandikwa juu
ya kikao hiki kwa watu ambao wanajifanya wapiga ramli, ila naomba
muyapuuze, ila ya kweli ni haya nitakayoongea.

“Kanda ya Pwani nilipata habari kuna
watu walinifuata nigombee Uenyekiti Kanda, nongwa ilikuja baada ya mimi
kuamua kugombea Uenyekiti Taifa, ila lengo la kwanza nilitaka kuondoa
hisia kuwa ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia ya kweli.

“Niliwaambia wajumbe kuwa mkifanya kama
mlivyotaka kufanya, nitauthitibitishia umma kuwa ndani ya CHADEMA hakuna
demokrasia ya kweli, au kiti cha Mbowe kina utaratibu mwingine.

“Nafasi ya Mwenyekiti Mbowe haiguswi
mimi nilitaka kuonesha kuwa hilo sio kweli lakini nilikuwa najidanganya
nimefanyiwa figisu kwenye uchaguzi wa kanda kisa niligusa kiti cha
Uenyekiti Taifa.

“Mbowe aliwahi kutupa nasaha kuwa
tusiionje sumu kwa kuilamba, na mimi siwezi kuigusa sumu kwa kuilamba
leo natangaza rasmi kuwa sitoendelea kugombea kwenye nafasi ya Uenyekiti
Taifa CHADEMA.

“Nimefedheheka sana kwa kitendo kilichofanywa hasa kwa kujua nimefanyiwa hivi kwasababu ya kukigusa kiti cha Uenyekiti Taifa.

“Kama wakubwa wameamua kuwashawishi
wapiga kura wangu wa Kanda ya Pwani hata kwa kuwaficha Hotelini, hii
maana yake naambiwa Sumaye akufukuzae akuambii toka.

“Baada ya kutafakari kwa kina, ustaarabu
unasema toka sasa hutakiwi, wako watakaosikitika nimelazimika kujiondoa
CHADEMA kutoka leo hii, mimi sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na
chama chochote, ila niko tayari kutumika na chama chochote.

“Najua katika kujikosha yatakuwepo
maneno Kama kapewa fedha na CCM au ACT n.k, kama nilipokuja CHADEMA
nilipewa pesa basi na safari hii nimepewa fedha ingawa sijui na nani
maana sijiungi na Chama chochote.

“Na kama nilikuja CHADEMA kwa hiari
yangu bila kupewa pesa basi na safari hii sijapewa pesa na sitopewa pesa
maana sijiungi na Chama chochote, mimi sijawahi kuwa Kibaraka wa Mtu
wala Kikundi na hata siku moja sitokuwa hivyo