Chadema waitaka serikali kutotumia jina na nembo ya chama chao kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa

Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetaka Serikali kutotumia
nembo na jina la chama hicho kwenye karatasi za kupigia kura katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu.


Naibu
Katibu Mkuu (Bara), wa chama hicho, John Mnyika amesema amesema hayo
leo Jumapili Novemba 10, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na
waandishi wa habari.

Amesema
sababu ya uamuzi huo ni kutokana na wao kujiengua katika kinyang’anyiro
hicho hivyo wagombea wao wasiwepo katika fomu hizo za kupigia kura.

“Kesho
Novemba 11, tutamuandikia barua Waziri wa Tamisemi (Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa), Suleiman Jaffo, kuacha kutumia jina nembo ya chama
chetu.

“Pia
tunamuomba Rais Dk. John Magufuli, kuingilia kati ukiukwaji wa sheria
unaoendelea kwenye uchaguzi huo kama alivyohamasisha wakati wa
uandikishaji,” amesema Mnyika.