Chadema wapewa saa mbili kuondoa bendera zao barabarani dar

Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic ameiandikia barua CHADEMA na
kuipa saa mbili kuondoa bendera zake zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma
karibu na ukumbi wa Mlimani City.

Bendera hizo ziliwekwa takriban
wiki mbili zilizopita ulipoanza Uchaguzi wa Mabaraza ya chama hicho huku
Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa chama hicho ukitarajiwa kufanyika kesho
Mkurugenzi huyo amesema Manispaa
ya Ubungo ndio inayoihudumia barabara hiyo inashangazwa kuona bendera za
chama hicho zikiwa kwenye bustani
Katika barua ya Mkurugenzi huyo
kwenda kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Vicent Mashinji, amesema bendera
zimewekwa kama matangazo kinyume na utaratibu wa kibali
Aidha, Meya wa Ubungo ambaye pia
ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Boniface Jacob amesema, “bendera
hizo haziondolewi kwa sababu CHADEMA tuna haki ya kutumia maeneo ya wazi
ya Umma kama vyama vingine vya siasa kwa mujibu wa sheria.”