Na Amiri kilagalila-Njombe
Chama
cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Njombe,kimetoa wito kwa
wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
linalotarajia kuanza disemba 30,2019 mpaka januari 5,2020 mkoani humo.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Njombe Rose Mayemba wakati akizungumza na vyombo vya habari.
“Tunafahamu
kwamba wananchi wamekatishwa tamaa sana na zoezi lililopita kwenye
serikali za mitaa,wengi ile hari imekufa, lakini nitoe rai kwa wananchi
wasiache wajibu wao wa kwenda kujiandikisha” alisema Rose Mayemba
Mwenyekiti
Rose Mayemba amewaagiza viongozi wa chama hicho kuto kuacha
kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha mara baada zoezi hilo
kukamilika katika maeneo mengine ya nchi na sasa zoezi hilo linatarajia
kuanza mkoani humo.

Aidha
amesema kama vilivyowekwa vipaumbele vya chama hicho ikiwemo kudai tume
huru ya uchaguzi,chama hicho hakitaweza kwenda kwenye uchaguzi bila ya
kuwa na tume huru.