Chuo cha sayansi za afya kolandoto chatoa msaada wa vitu mbalimbali wa wazee shinyanga

Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kimetoa msaada wa chakula na vitu
mbalimbali katika kituo cha Makazi ya  Wazee na wasiojiweza Kolandoto kilichopo Manispaa
ya Shinyanga.

Vitu vilivyotolewa ni pamoja na Mchele, Maharage, Mafuta ya kupikia, Mafuta
ya kujipaka, Sukari,unga wa sembe, Sabuni za kufulia, Miswaki na mbuzi wawili
kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka kwa mwaka huu 2023.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi
za Afya Kolandoto Bwana Michael Henerco ameiasa jamii, viongozi mbalimbali na
wadau kwa ujumla kuwa na moyo wa majitoleo kwa watu wenye uhitaji ili kuendelea
kupata baraka za mwenyezi Mungu.

“Tunapokuja hapa tutambue kuwa ni wajibu watu
na kwamba mambo tunayoyafanya hapa tutambue kwamba tunatakikana kuyafanya
kwahiyo kuja hapa ni tone kwa maana ya kwamba ni kupata chachu ya kukumbuka
kuendelea kuwakumbuka wazee popote unapokutana nao, panga tu katika familia
yako kufanya mambo ya kiibada kama haya siyo lazima sana uje kwenye kituo kama
tulivyofanya  sisi”.

“Wafundishe watoto wako kufanya matukio ya
kiibada kwa wazee na watu wengine wasiojiweza wakikutana nao kwa sababu
utakapofika muda na wewe unahitaji kupata msaada kama watoto wako hukuwafundisha
usitegemee watakusaidia, kwahiyo niendelee kuwasisitiza kuwa moyo huu tuendelee
kuwa nao na tuufanye kwa uthabiti sana nasisi chuo cha Sayansi za Afya
kolandoto tumeanza na tunaendelea wazee pamoja na watu wengine wenye uhitaji”.
amesema Kaimu mkuu wa chuo bwana Henerco

Kwa upande wake Afisa Mfawidi wa kituo cha Makazi ya  Wazee na wasiojiweza Kolandoto Bi. Sophia
Kang’ombe ameshukuru kwa msaada huo na kubainisha kuwa kituo hicho bado
kinauhitaji ambapo amewaomba viongozi katika taasisi mbalimbali na wananchi kwa
ujumla kuguswa kwa majitoleo ili kupunguza au kumaliza kabisa changamoto
zilizopo.

“Nakushukuru sana kaimu mkuu wa chuo pamoja na
timu nzima yako ya watumishi kwa kuweza kuguswa kutuletea zawadi ya Pasaka kwa
wazee wetu kwa kweli Mungu awabariki kwa jambo hili nawaomba tuendelee
kushirikiana siku zote”.

“Na nitoe wito kwa wadau wengine wa nadani na
nje ya Mkoa wa Shinyanga tunamahitaji mengine ambayo bado wazee wetu wanahitaji
tofauti na chakula tunahitaji kupata jengo lingine kubwa ili wazee wetu waweze
kupata nafasi ya kutosha kukaa kila mmoja kwenye chumba chake bado tunawaomba
wadau popote pale walipo karibuni muweze kuunga juhudi za serikali katika
kuwatunza wazee”.
amesema Bi.
Sophia Kang’ombe

Nao baadhi ya wazee hao wameshukuru kwa msaada huo ambao utawasaidia kupunguza
 changamoto mbalimbali zilizokuwa
zinawakabili.

 

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto
Bwana Michael Henerco akizungumza katika hafla hiyo.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto
Bwana Michael Henerco akizungumza katika hafla hiyo.

Afisa Mfawidi wa kituo cha Makazi ya  Wazee na wasiojiweza Kolandoto Bi. Sophia
Kang’ombe akizungumza katika hafla hiyo.

 

Hafla ya kukabidhi msaada wa chakula na vitu mbalimbali ikiendelea leo
April 5,2023 katika kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto Mkoani
Shinyanga 





 Mwalimu mkufunzi idara ya uuguzi Kolandoto College of Health Science (Afisa muuguzi) Elikana Wallace upande wa kulia akitoa elimu juu ya ugonjwa wa Kisukari.

Wazee na wasiojiweza kituo cha Kolandoto wakiendelea kupima juu ya ugonjwa wa kisukari




Zoezi la vipimo juu ya ugonjwa wa kisukari likiendelea katika kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto likiendelea katika hafla ya kukabidhi msaada.