KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, akiwahutubia Wana CCM katika uzinduzi wa
kampeni ya Magharibi ya Kijani iliyozinduliwa katika ukumbi wa Chuo cha
kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu Zanzibar.

Dkt.Bashiru Ally Kakurwa,akitembelea vikundi vya wajasiriamali
walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa Magharibi ya Kijani Zanzibar.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa
Magharibi kichama ndugu Mohamed Rajab Soud, akizungumza katika hafla
hiyo ya uzinduzi wa kampeni ya magharib ya kijani iliyofanyika Bububu
Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Zanzibar.

::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, ameyaonya
mashirika ya kimataifa yanayowakilisha nchi zao Tanzania kuacha
kuingilia siasa za ndani ya nchi.

Alisema
kuna baadhi ya wawakilishi wa nchi hizo za kigeni wameanza kutoa kauli
zisizofaa na vipeperushi kupitia nchi za mitandao wakibeza na kuhoji
kuhusu Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.

Hayo
aliyasema wakati akizindua kampeni ya Magharibi ya kijani huko katika
ukumbi wa Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Zanzibar.

ajenda ya uchaguzi huo tayari imefungwa na chama cha mapinduzi kimeibua
mshindi kwa asilimia zaidi ya 99 na kwa sasa kinajipanga na Uchaguzi
Mkuu ujao wa mwaka 2020.

watu hao wanaojadili uchaguzi katika mitadao ya kijamii ni kupoteza
muda kwani mitandao haipigi kura wala kubadilisha uhalisia wa ushindi
wa CCM.

“Naendelea
kuwakumbusha hawa wenzetu wanaojadili uchaguzi katika mitandao kuwa
Whatsapp na Instagram na facebook hazipigi kura na hazijasajiliwa katika
daftari la kudumu la wapiga kura”, amesema Dkt.Bashiru.

Katika
maelezo yake Dkt.Bashiru alisema kuna baadhi ya watu wanadhani
demokrasia ipo katika uchaguzi tu jambo ambalo sio sahihi kwani hata
kutokuwa na tama ya kukandamiza uhuru wa wengine pia ni demokrasia.

Akizungumzia
kampeni hiyo iliyozinduliwa alisema kampeni ya kijani iliyoasisiwa na
UVCCM imesaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha shughuli za kisiasa ndani
ya Chama na Jumuiya zake.

kampeni hiyo ya Magharibi ya kijani inatakiwa kutoa matokea chanya
yanayoendana na malengo yaliyokusudiwa na kuimarisha shughuli za kisiasa
chama ndani ya mkoa huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alieleza
kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964 ndio
yaliyofanikisha nchi kujitawala na kufikia maendeleo endelevu yaliyopo
hivi sasa.

Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020,alisema imetekelezwa kwa
ufanisi mijini na vijiji wanapata huduma bora za kijami,kiuuchumi na
kimaendeleo bila ubaguzi.

Dkt.Bashiru,
alihoji wanaobeza uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
ambaye anamaliza muda wake mwaka ujao akiwa na historia nzuri na
iliyotukuka ya uchapakazi na uadilifu.

Dk.Shein ni kingozi mwenye uzoefu na uwezo mkubwa kiuongozi kwani
amehudumu kwa muda mrefu ndani ya ngazi za juu za Chama na Serikali.

Rais ajaye wa Zanzibar anatakiwa kuwa na sifa kama za Rais wa
sasa Dk.Ali Mohamed Shein ambaye ni muadilifu,mpole na mchapakazi.

“
Nawashangaa baadhi ya wanasiasa eti wanatathimini Dk.Shein na Serikali
anayoiongoza nawambia kuwa Rais huyu ni wa kuigwa kwani mambo ya
maendeleo aliyoyafanya Zanzibar yanaonekana kwa kila mtu”, alieleza na
kuongeza kuwa Rais huyo hadi hivi sasa hana kashifa za rushwa wala
ufisadi.

Pamoja
na hayo Dkt.Bashiru, aliwasihi Wana CCM kuendelea kushikamana na
kulinda uhuru ulioasisiwa na Waasisi wa Chama hicho kwa gharama yoyote
bila hofu.

Katibu
huyo alisema ushindi uliopatikana katika uchaguzi wa serikali za mitaa
Tanzania bara ni sehemu ya kutesti mitambo na kwa sasa anatumia ziara
yake kuendelea kufunga mitambo katika Mikoa yote ya Zanzibar ili 2020
CCM ipate ushindi wa kihistoria.

Aliahidi
kwamba akiwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ndani ya CCM kwa Tanzania nzima
atahakikisha CCM inashinda Zanzibar na Tanzania bara katika uchaguzi
mkuu ujao.

Naye
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mwl.Kombo Hassan Juma, alisema
CCM inaimarika kisiasa kutokana na Serikali kutekeza vizuri Ilani ya CCM
.

Mapema
akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharib ndugu Mohamed Rajab
Soud,alisema kampeni hiyo imezinduliwa kwa lengo la kusafisha njia ya
kisiasa kuelekea 2020.