Dkt kyaruzi aridhishwa na uzalishaji umeme kituo cha new pangani falls

Mhandisi
Uzalishaji wa Kituo cha New Pangani Falls Dalali Mnyamiru kushoto
akionyesha namna mitambo inayofanya kazi kwenye kituo hicho wakati wa
ziara ya Bodi ya wakurugenzi kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt
Kyaruzi


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt Kyaruzi kulia akitazama utendaji kazi wa mitambo ya kufufua umeme wa gridi ya Taifa katika kituo cha New Pangani Falls kilichopo Hale wilayani Korogwe kushoto ni Mhandisi Uzalishaji wa Kituo cha New Pangani Falls Dalali Mnyamiru

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt
Kyaruzi kulia akisisitiza jambo mara baada ya kutazama

utendaji kazi wa mitambo ya kufufua umeme wa gridi ya Taifa
katika kituo cha Pangani kilichopo Hale wilayani Korogwe
Mhanidisi Uzalishaji wa Kituo cha New Pangani Falls Dalali Mnyamiru  kulia akieleza jambo wakati wa ziara hiyo

MWENYEKITI  wa Bodi ya
Wakurugenzi wa TANESCO Dkt Alexander Kyaruzi amesema kwamba ameridhishwa na mitambo
inayotumika kuzalishia umeme ilivyopo kwenye kituo cha New Pangani Falls
kilichopo Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

Hayo aliyasema leo wakati
wa ziara ya siku moja ya kutembelea mitambo hiyo ambapo alisema kwamba hali ya
mitambo hiyo ni nzuri na inauwezo wa kuzalisha umeme unaostahili

Alisema kwamba katika
ziara hiyo lengo lao ni kutaka kuona namna kituo hicho kinavyofanya kazi
kutokana na kwamba tokeo bodi hiyo ilipochaguliwa haijawahi kufika kwenye
mitambo hiyo

“Kwa
kweli leo
nimefika hapa kufanya ziara lakini kikubwa nataka kusema nimeridhishwa
sana na
mitambo inayotumika kuzalishia umeme hapa kwani kuna mitambo mitatu ya
Hale, Nyumba
ya Mungu na Pangani Falls kama bodi ambao tunasimamia haya mambo ni
vizuri tumeona tuje kujielimishe na ndio maana tumefika”Alisema Dkt
Kyaruzi.

Alisema kwamba baada
ya kufika wamepata uelewa kwamba wana mashine mbili ambazo kila moja inazalisha
megawatts 34 hivyo kufanya jumla yake kuwa megawatts 68 na mashine zote mbili
zinafanya kazi kwa kiwango kizuri.

Akielezea changamoto ambazo
alihaidi kwenda kuzipatia ufumbuzi ambazo alielezwa wakati wa ziara hiyo,Mwenyekiti
huyo wa Bodi ya Wakurugenzi alisema ni pamoja na ile ya kwamba mitambo yao ipo
kwenye bonde la Mto Pangani ambao una mamlaka yake ambalo ameliona linaweza
kuwa ni tatizo kidogo.

Alisema hilo
linatokana na kwamba mamlaka yenyewe inatilia kipaumbele uzalishaji wa
umwagiliaji ndio wa kwanza halafu uzalishaji umeme ni kipaumbele namba mbili sasa
hilo linawafanya wao kama TANESCO wasiweze kupanga kwa kuangalia maji yaliyopo
bwawani.

Alieleza kwamba kwani
hayo maji wanaweza kuyatumia kwa mwaka mzima sasa kama wengine wanapewa
kipaumbele wao wanaweza kuwa wamepanga kumbe kipaumbele kimebadilika kwa wale
wengine na hivyo kupelekea kushindwa kufika mwaka mzima.

 “Hili tumeona hivyo tumepanga ni vizuri tukawa na mawasiliano
na wenzetu wa bonde la Mto Pangani angalau tuweze kuwa na vipaumbele sawa kurahisisha
kwenye mambo ya kupanga”Alisema

Mwenyekiti huyo wa
Bodi ya Wakurugenzi alisema nyengine walioona kama changamto ni udongo wamewaeleza
kwenye mabwawa udongo na mchanga upo mwingi hiyo kusababisha maji yanayokaa
pale ndani yanapungua kina chini .

Alieleza kwamba hilo
linasababishwa na uwepo wa udongo na mchanga na kupelekea maji yanapungua hiyo ni changamoto ambayo
wanaichukua na kuona namna ya kuifanyia marekebisho jinsi ya kuuondoa huo
mchanga na tope ili bwawa liweze kuwa na kina cha zamana kama kilivyosanifiwa.